Header Ads

SAMATTA AFUNGA GOLI LAKE LA KWANZA PREMIER LEAGUE

NYOTA ya mshambuliaji wa Tanzania, Mbwana Samatta anayeichezea klabu ya AstonVilla inayoshiriki Ligi Kuu England, imezidi kupaa baada ya kuanza katika mchezo wao wa leo Jumamosi  wa Ligi Kuu dhidi ya AFC Bournemouth utakaoanza saa 12:00 jioni.

Huu unakuwa ni mchezo wa pili upande wa Samatta kuichezea timu hiyo, huku awali akiwa ameanza katika mchezo wa kombe la Carabao dhidi ya Leicester City na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 huku yeye akiwa amecheza dakika 67.

AstonVilla watakuwa ugenini kuwakabili Bournemouth uwanja wa Vitality ambao unachukua takribani mashabiki 11,329, hivyo Samatta atakiongoza kikosi chake kuhakikisha wanatoka na ushindi kwenye mchezo huo.

Mchezo huu unakuwa wa kukatana shoka kwa timu zote kutokana na kwamba zote zipo nafasi mbaya kwenye msimmao hivyo kila mmoja anahitaji ushindi ili kusogea juu.

Bournemouth ambao wapo nyumbani wanashika nafasi ya 17 wakiwa na pointi 23 katika michezo 24 waliyocheza huku Villa wakishika nafasi ya 16 wakiwa na pointi 25 katika michezo 24 waliyocheza.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!