Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

KAMPUNI YA PETROBENA YAOMBWA KUOKOA ZAO LA MAHINDI TABORA.

 WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA WA 27 WA CHAMA KIKUU CHA WAKULIMA WA TUMBAKU KANDA YA MAGHARIBI (WETCO) WAKIWA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO.

TABORA:
Wakulima wa Tumbaku mkoani Tabora wameiomba kampuni ya Usambazaji wa Pembejeo ya Petrobena kuwasambazia mbolea ya UREA  kwa ajili ya kilimo cha mahindi kwani zao hilo linawasaidia kupata chakula.

Wakiongea katika mkutano wa mkuu wa 27 wa chama kikuu cha wakulima wa Tumbaku kanda ya Magharibi (WETCU) baadhi ya wakulima wamesema kuwa uzalishaji wa mahindi ni mdogo hali inayosababisha familia nyingi kukosa chakula cha uhakika.

Wameongeza kuwa kilimo cha Tumbaku kinahitaji nguvu kazi na nguvukazi inahitaji Chakula hivyo kukosa mbolea ya mahindi kunasababisha nguvu kazi hiyo kushindwa kufanya uzalishaji mzuri wa Tumbaku.

Katika mapendekezo yao wakulima hao wameomba kupatiwa mifuko miwili ya UREA kwa heka moja na kwamba hali hiyo itasaidia kupata mahindi mengi ambayo yatasaidia kwa chakula katika familia zao.

Katika hatua nyingine wakulima hao wameomba kufanyiwa tathimini ya idadi ya heka za mahindi wanazolima kwa kila kaya kama wanayofanyiwa kwenye Tumbaku ili kujua idadi za mbolea ambazo watakopeshwa ili kuinua zao hilo.

MATUKIO KATIKA PICHA:

WAFANYAKAZI WA WETCO PAMOJA NA WAGENI KUTOKA MAKAMPUNI MBALI MBALI WAKIWA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO.

 MKUTANO UKIENDELEA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA AGRIANA MKAONI TABORA.

 WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA WA 27 WA CHAMA KIKUU CHA WAKULIMA WA TUMBAKU KANDA YA MAGHARIBI (WETCO) WAKIWA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO.

 MRAJISI WA VYAMA VYA USHIRIA MKAI TABORA AKITOA HOTUBA YAKE KATIKA MKUTANO MKUU WA 27 WA WETCU.

 MKUU WA MKOA WA TABORA AGGREY MWANRI AMBAYE ALIKUWA MGENI RASMI KATIKA MKUTANO WA 27 WA CHAMA KIKUU CHA WAKULIMA WA TUMBAKU (WETCO) AKITOA HOTUBA KWA WAKULIMA WA VYAMA VYA MSINGI.

 AFISA WA TAKUKURU MKOA WA TABORA MUSSA CHAULO AKITOA ELIMU KUHUSU RUSHWA NA MADHARA YAKE KATIKA VYAMA VYA USHIRIKA.

 MKUTANO MKUU WA 27 WA WETCU TABORA UKIENDELEA KATIKA UKUMBI WA AGRIKANA TABORA.

 MWENYEKITI WA BODI YA TUMBAKU TANZANIA HASSAN WAKASUBI AKIONGEA NA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA WETCU,KIKUBWA AMEWATAKA WAKULIMA KUHESHIMU MAKISIO WANAYOINGIA NA MAKAMPUNI.

MENEJA MKUU WA WETCO TABORA AKIONGOZA AJENDA KATIKA MKUTANO HUO.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News