Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

SERIKALI WILAYANI KAHAMA KUWACHUKULIA HATUA KALI WASIOSAFISHA MITARO


Serikali wilayani Kahama mkoani Shinyanga imesema itaanza  kuwachukulia hatua za kisheria  wananachi watakaoshindwa kusafisha mitaro  inayopitisha maji katika barabara zote za mitaa kwa kuwa uchufu unaorundikana unasabanisha kuharibu miundombinu ya barabara.
Kauli hiyo imetolewa  Jana na mkuu wa wilaya ya  Kahama Anamringi Macha wakati akikagua mitaro iliyohaririwa kwa mvua, katika mtaa wa Mayila mjini Kahama  na kusema kuwa ni wajibu wa kila mwenye nyumba kusafisha mitaro ikiwamo kutoa mchsnga na udongi kwenye mitaro hiyo.
Amesema serikali haitasita kuchukua  hatua ikiwamo kufunga vibanda by biashara kwa wanchi ambao watashindwa kutekeleza na kwamba viongozi wa serikali ya mtaa wasimamie Jambo Hilo.
Baadhi ya wananchi waliozungumza wamesema wamelipokea agizo la serikali ingawa wanaomba  mitaro injengwe kila upande wa barabara ili   kumudu Kasi ya kuyapokea maji yanayopita  katika barabara za mitaa.
Barabara nyingi za mitaa  mjini Kahama zimeharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, huku mitaro iliyongengwa katika baadhi ya barabara umeharibika kutokana na kukithiri kwa takataka, mchanga na udongo Hali inayosababisha maji kupita kwenye baraba na kusababisha kuharibika.


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News