Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

MAAFISA USHIRIKA WATAKIWA KUSIMAMIA VYAMA VYA MSINGI NA KUACHA KUWADIDIMIZA WAKULIMA.

MWENYEKITI WA TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA NCHINI (TCDS) DOKTA. TITUS KAMANI
GEITA
Serikali imewataka maafisa ushirika  katika halmashauri zote nchini kusimamia kikamilifu   vyama vya Msingi kwa kutoa ushauri wenye tija badala ya kuwadidimiza wakulima na kusababisha  hasara kubwa kwa wakulima na serikali kwa ujumla.


Kauli hiyo imetolewa jana na mwenyekiti wa tume ya maendeleo ya ushirika nchini (TCDS) Dokta. TITUS Kamani kwenye mkutano mkuu wapili wa chama kikuu cha ushirika mbogwe na bukombe (MBCU) kilichofanyika katika wilaya ya mbogwe mkoani geita.

Amesema  Serikali imeibosha Sheria ya Ushirika  na  kwamba kwa sasa usimamizi na matumizi ya mali za vyama vya msingi na Ushirika  vinasimamiwa na  Maafisa Ushirika wa kila wilaya hivyo serikali haitegemei kuona hasara unaotokana na upoptevu wa mali mbalimbali vya vyama vya Msingi.

Mkuu wa wilaya ya mbogwe MATHA  MKUPASI amesema mwaka huu wakulima watazalisha kwa wingi  baada ya kupata pembejeo kwa wakati kutoka kwa  kampuni ya  Petrobena  inayojihusisha na  masuala ya pembejeo kwa wakulima Kuondoa urasimu ulikuwepo hapo awali.

Mmoja wa wakulima wa Tambaku CATHERIN AGUSTINO ameziomba taasisi za fedha kuacha ubaguzi katika utoaji wa mikopo kwa baadhi ya amcos huku samwel nalumbike afisa kilimo na ushirika wilaya ya mbogwe, akiwataka wakulima kutumia pembejeo bora ambazo haziharibu ardhi.

MATUKIO KATIKA PICHA:

MKUU WA WILAYA YA MBOGWE MARTHA MKUPASI AKIFUNGUA MKUTANO WA PILI WA CHAMA CHA MBCU.

 WAGENI KUTOKA TAASISI MBALI MBALI WAKIWA KATIKA MKUTANO HUO.

 WADAU WA PETROBENA WAKIFUATILIA KWA MAKINI MKUTANO HUO ULIOFANYIKA MBOGWE.

 WAKULIMA KUTOKA CHAMA KIKUU CHA WAKULIMA MBCU WAKIFUATILIA KWA MAKINI MAELEZO YA MGENI RASMI.


 WAKULIMA KUTOKA CHAMA KIKUU CHA WAKULIMA MBCU WAKIFUATILIA KWA MAKINI MAELEZO YA MGENI RASMI.

 MUWAKILISHI WA KAMPUNI YA PETROBENA BONIFACE KAVISHE AKIFUATILIA KWA UMAKINI MKUTANO WA PILI WA CHAMA CHA USHIRIKA MBCU. VIONGOZI WA MBCU WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WADAU NA TAASISI

MKUU WA WILAYA YA MBOGWE MWENYE MIWANI KATIKATI AKIBADILISHANA MAWAZO NA WAKULIMA WA MBOGWE NA BUKOMBE.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News