Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

WAISLAMU WA KI-IBADHI KAHAMA KWA KUSHIRIKIANA NA JUMUIYA YA KIISLAMU YA ISTIQAAMA YA NCHINI OMAN YATOA MSAADA KWA WAGONJWA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA.KAHAMA
Mashirika yasiyo ya kiserikali,Taasisi na Watu binafsi wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameombwa kujitokeza kuwasaidia wagonjwa wasiojiweza mahospitalini kwani baadhi yao hawana ndugu wakuweza kuwasaidia.

Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Masjid Al-wahabu Mohamed Issa Hilaly Al-Habsy wakati akikabidhi msaada kwa niaba ya jumuiya ya Internatioanl istiqumaa Muslim Community  ya nchini Oman katika hospitali ya wilaya ya Kahama.

Al-Habsy amesema kuwa ukimsaidia mtu mwenye matatizo mtu Yule akashukuru kwa ulichotoa hivyo mwenyezi Mungu atakujulia mema katika shughuli zako na familia yako.

Kwa upande wake katibu wa Masjid Al-wahabu Shehe Ahmed Haroun Al-Nuby amesema kuwa msaada huo wameulenga sana kwa watu ambao hawajiwezi,na kwamba wameona kuna umuhimu wa kuwasaidia wanyonge.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mganga mkuu, Mganga wa zamu katika hospitali hiyo Adam Masaguda ameishukuru jumuiya ya kiislamu ya Istiqamaa kwa msaada huo na kuongeza kuwa katika hospitali hiyo kuna wagonjwa wengi wanaohitaji msaada kwani kuna wengine hawana ndugu .

Kwa upande wao baadhi ya wagonjwa na waangalizi wa wagonjwa waliopata msaada huo wameishukuru jumuiya ya Internatioanl istiqumaa Muslim Community  ya nchini Oman kwa msaada huo na kwamba imewapunguzia gharama za matumizi kwa kiasi kikubwa.

 MATUKIO KATIKA PICHA:


BAADHI YA MISAADA AMBAYO IMEKABIDHIWA KWA WAGONJWA LEO KUTOKA KWA WAISLAMU WA KI-IBADHI KAHAMA

 MANDALIZI YA MAKABIDHIANO BAADA YA KUFIKISHA MSAADA HUO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA.

KATIBU WA MASJID AL-WAHAB SHEHE AHMED AL-NUBY KUSHOTO AKIKABIDHI MISAADA HIYO.

MAKABIDHIANO YA MISAADA MBALI MBALI YAKINDELEA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA.

 KATIBU WA MASJID AL-WAHAB SHEHE AHMED AL-NUBY KUSHOTO AKITOA NENO KABLA YA KUKABIDHI MSAADA HUO.

 MWENYEKITI WA MASJID AL-WAHAB MOHAMED AL-HABSY KUSHOTO AKISISITIZA JAMBO KUWATAKA WAHISANI WENGINE KUJITOKEZA KUTOA MSAADA KWA WAGONJWA WASIOJIWEZA.

 MGANGA WA ZAMU KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA ADAM MASAGUDA KUSHOTO AKITOA SHUKRANI MARA BAADA YA KUPOKEA MSAADA HUO.

 WAUGUZI WALIO KATIKA MAFUNZO YA VITENDO,WAKISAIDIA KUPELEKA MISAADA HIYO WODINI.

 MISAADA IKIPELEKWA WODINI KWA AJILI YA KUWAGAWIA WAGONJWA.

 MISAADA MBALI MBALI IKIPELEKWA WODINI KWA WAGONJWA.

 WAISLAMU WA KI-IBADHI WAKIPELEKA MISAADA KWENYE WODI YA WATOTO.

 ZOEZI LA UGAWAJI LIKIENDELEA KATIKA WODI YA WAZAZI,HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA.

MWENYEKITI WA MASJID AL-WAHAB MOHAMED AL-HABSY AKISOMA DUA KWA AJILI YA KUWAOMBEA WAGONJWA KATIKA WODI YA WANAWAKE,HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA.

 SAFARI YA KUGAWA MISAADA ILIKUWA NI WODI KWA WODI,HAPA WAKIELEKE WODI YA MAJERUHI KUGAWA MSAADA HUO.

 SAFARI YA KUGAWA MISAADA ILIKUWA NI WODI KWA WODI,HAPA WAKIELEKEA WODI YA WATOTO KUGAWA MISAADA.

 ZOEZI LA UGAWAJI MISAADA LIKIENDELEA KATIKA WODI MBALI MBALI KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA.

ZOEZI LA UGAWAJI  MSAADA LIKIENDELEA.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News