Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

KIWANDA CHA USHONAJI CHA KINA MAMA WA KI-BADHI CHAFUNGULIWA ISAKA KAHAMA,

WANAWAKE WA KI-IBADHI KATIKA MRADI WA KUSHONA ISAKA KAHAMA WAKIWA KATIKA CHEREHANI ZAO WALIZOKABIDHIWA.
KAHAMA
Wanawake mafundi Cherehani katika mji wa Isaka Wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameishukuru jumuiya ya Internatioanl istiqumaa Muslim Community  ya nchini Oman kwa kuwapa msaada ya Vyerehani hali itakayowafanya waondokane  kushona kwa kutumia Vyerehani vya kukodi.

Wakiongea mara baada ya kukabidhiwa vyerehani hivyo wanawake hao wamesema kuwa walikuwa hawana uwezo wa kununua vyerehani   na kwamba kwasasa wataweza kujisimamia na kujikimu katika maswala mbali mbali ya Familia.

Katika hatua nyingine wanawake hao wameomba wafadhili wengine kujitokeza kuwapa msaada wa vitambaa,kwani kiwanda chao ni kipya na hakina uwezo wa kununua malighafi kama majola ya vitambaa ili kujiendesha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Isaka Rajab Kaombwe   ameishukuru  jumuiya hiyo kwa msaada wa Vyerehani hivyo na kuwaomba wafadhili kufikisha mradi huo katika maeneo mbalimbali huku akiwataka wanawake wa Isaka kutunza Vyerehani hivyo.

Awali akikabidhi Vyerehani hivyo kwa niaba ya Wafadhili Mzee wa Kii-badhi kutoka Halmashauri ya Mji wa Kahama Mohamed Malik amewataka wanawake hao kuzitunza Cherehani hizo na kuwa wamoja  na kuwataka kupeleka cherehani zingine katika vijiji jirani ili kuufanya mradi huo uwe mkubwa.


Jumuiya ya Internatioanl istiqumaa Muslim Community  ya nchini Oman imeendelea kuunga mkono Juhudi za Serikali ya awamu ya Tano ya kukuza uchumi wa Viwanda kwa kutoa Msaada wa Vyerehani 15 na jengo la ushonaji vyote vikiwa na gharama ya Shilingi milioni 15 za kitanzania kwa ajili ya kufungua kiwanda cha Ushonaji kwa wanawake wa Kijiji cha Isaka halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

MATUKIO KATIKA PICHA:

 WANAWAKE WA KI-IBADHI KATIKA MRADI WA KUSHONA ISAKA KAHAMA WAKIKAGUA CHEREHANI ZAO WAKISIMAMIWA NA WALEZI WAO.


 WANAWAKE WA KI-IBADHI KATIKA MRADI WA KUSHONA ISAKA KAHAMA WAKIMSIKILIZA MZEE MZEE WA KI-IBADHI KUTOKA KAHAMA MJINI MOHAMED MALIK AMBAYE HAYUPO PICHANI.

 WAISLAMU WA KI-IBADHI WAKENDELEA KUTOA WOSIA KWA WANAMAMA WALIOPATIWA CHEREHENI HIZO JUU YA MATUMIZI NA UTUNZAJI.

 HILI NDILO JENGO AMBALO WAKINA MAMA WA KI-IBADHI WAMEJENGEWA NA JUMUIYA YA KIISLAMU YA INTERNATIONAL ISTIQAMAA MUSLIM COMMUNITY KWA AJILI YA SHUGHULI ZAO ZA USHONAJI.


 MZEE WA K-KIBADHI KUTOKA KAHAMA MJINI MOHAMED MALIK MWENYE KANZU NYEUPE KULIA AKIONGEA NA WANAMAMA HAO WAKATI WA KUWAKABIDHI CHEREHANI .

 MZEE WA K-KIBADHI KUTOKA KAHAMA MJINI MOHAMED MALIK AKIKATA UTEPE KUASHIRIA UFUNGUZI RASMI WA JENGO LA MRADI WA KUSHONA KWA WANA MAMA WA KI-IBADHI ISAKA KAHAMA.


 WANAWAKE WA KI-IBADHI ISAKA WAKIWA WAMEKAA KWENYE CHEREHANI ZAO WAKIMSUBIRI MGENI RASMI KUZINDUA RASMI MRADI HUO.
HUU NDIYO MWONEKANO WA JENGO LA MRADI WA KUSHONA KWA WAMAMA WA KI-IBADHI KATIKA ENEO LA ISAKA HALMASHAURI YA MSALALA WILAYANI KAHAMA MKOANI SHINYANGA.


MZEE MOHAMED MALIK AKIKAZIA JAMBO KWA WAMAMA WA KI-IBADHI 

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News