Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

JUMUIYA YA KIISLAMU YA AL TIJARAH AL RABIHA YA OMAN YAJENGA ZAHANATI YA KISASA KAHAMA.


WAGENI KUTOKA JUMUIYA YA KIISALMU YA AL TIJARAH AL RABIHA YA OMAN WAKIWA NA WENYEJI WAO KATIKA UZINDUZI WA ZAHANATI YA MASCUT.

KAHAMA
Wito umetolewa kwa wananchi wilayani Kahama mkoani Shinyanga kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili kutambua maradhi yanayowasumbua na kupatiwa matibabu.

Hayo yamesemwa leo na Profesa Khalfan Al-Mandhari kutoka jumuiya ya Kiislamu ya Al Tijarah Al Rabiha nchini Oman wakati wa ufunguzi wa zahanati ya Mascut iliyopo mtaa Nyakato kata ya Nyasubi.

Profesa Khalfan amesema kuwa upatikaji wa Zahanati hiyo itasaidia jamii kupata huduma bila kujali itikadi ya dini wala makabila na kuitaka jamii kuitunza zahanati hiyo.

Akito shukrani kwa niaba ya wananchi Mtendaji wa kata ya Nyasubi Innocent Kapere ameishukuru taasisi hiyo kwa kujenga zahati hiyo na kwamba itasaidia kupunguza foleni katika hospitali ya wilaya ya Kahama.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Masjid Al-wahab Mohamed Alhabsy amewataka wananchi wa Kahama kuwa kitu kimoja katika kuitunza  zahanati hiyo ikiwa ni pamoja na kufika kutibiwa huku katibu wake Shehe Ahmed Al-Nuby akisema kuwa zahanati hiyo haibagui dini ya mtu.

Zahanati ya Mascut iliyopo Mtaa wa Nyakato kata Ya Nyasubi iliyozinduliwa leo imejengwa kwa ufadhili wa Jumuiya ya kislamu ya IAl Tijarah Al Rabiha nchini Oman na inatarajia kuanza kazi kuanzia jumatatu wiki ijayo.

 MATUKIO KATIKA PICHA:

MWONEKANO WA MOJA YA OFISI YA MGANGA KATIKA ZAHANATI HIYO.

        HIVI NDIYO VITANDA VYA WAGONJWA WAKATI WA KUPATIWA MATIBABU.

HAPA NDIPO SEHEMU AMBAPO HUDUMA YA DAWA ZITATOLEWA.

MWONEKANO WA JENGO LA ZAHANATI YA MASCUT NYASUBI.

WODI YA MAPUMZIKO KWA WAGONJWA.

BAADHI YA WAKAZI WA KAHAMA WALIOFIKA KATIKA UZINDUZI WA ZAHANATI HIYO WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA.

BAADHI YA MASHEHE WA KAHAMA WAKIWA TAYARI KUWAPOKEA WAGENI KUTOKA OMAN.

BAADHI YA MASHEHE WA KAHAMA WAKIWA TAYARI KUWAPOKEA WAGENI KUTOKA OMAN.

WAGENI KUTOKA OMAN WAKIZUNGUKA KATIKA JENGO HILO KUANGALIA UJENZI ULIVYOFANYIKA.

UKAGUZI WA MAJENGO UKIENDELEA.

MAZUNGUMZO YA PAMOJA YAKIFANYIKA KATI YA WAGENI NA WENYEJI KATIKA ZAHANATI HIYO.

WAGENI KUTOKA MAENEO MBALIMBALI WALIOFIKA KATIKA UZINDUZI WA ZAHANATI HIYO.

WAGENI KUTOKA OMAN WAKIMSIKILIZA SHEHE AHAMED AL NUBY HAYUPO PICHANI,

PROFESA  KHALFAN AL MANDHARI KUTOKA JUMUIYA YA KISLAMU YA AL TIJARAH AL RABIHA AKITOA NENO KWA WAGENI WALIOFIKA KATIKA UZINDUZI HUO.

MTENDAJI WA KATA YA NYASUBI INNOCENT KAPERE MWENYE SHATI JEKUNDU AKIWAKARIBISHA WAGENI NA KUWAPA HISTORIA YA KATA YA NYASUBI NA IDADI YA KAYA.

PROFESA  KHALFAN AL MANDHARI KUTOKA JUMUIYA YA KISLAMU YA AL TIJARAH AL RABIHA AKIONDOKA ENEO LA TUKIO MARA BAADA YA ZOEZI LA UZINDUZI KUISHA.

MWONEKANO WA NJE WA JENGO LA ZAHANATI YA MASCUT 


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News