Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

WABUNGE WANNE CHADEMA WANUSURIKA KWENDA GEREZANI....MAHAKAMA YAWAPA ONYO

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaonya wabunge wanne wa Chadema waliokiuka masharti ya dhamana kwa kutofika mahakamani bila taarifa yoyote.

Onyo hilo limetolewa leo Jumatano Novemba 20, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya kusikiliza utetezi wao


Wabunge hao ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya.

“Baada ya kupitia hoja za pande zote mbili na hoja za washtakiwa mahakama inaona kwamba maelezo yao hayana mashiko na kuwafutia dhamana ni hatua kali sana badala yake mahakama inawapa onyo kali wasirudie tena,” amesema Hakimu Simba.

Hakimu Simba amesema walifanya makusudi na kwamba hatua ya kujisalimisha polisi ni uoga wa jambo ambalo lingewatokea.

Kutokana na hali hiyo, amesema mahakama imewaachia kwa dhamana zao za awali na kuwataka wafuate masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili.

Novemba 15, 2019 mahakama hiyo iliamuru wabunge hao kukamatwa baada ya siku hiyo kukiuka masharti ya dhamana kwa kutofika mahakamani kusikiliza kesi ya uchochezi inayowakabili.

Wabunge hao walianza kujisalimisha kuanzia Jumamosi iliyopita na leo mahakama hiyo ilipanga kutoa uamuzi kuhusu kukiuka kwao dhamana.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Februari Mosi na Februari 16, mwaka huu Mbowe na wenzake wakiwa Kinondoni, Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama na  wengine ambao hawapo mahakamani ya kutenda kosa la jinai ikiwamo kuendelea na mkusanyiko isivyo halali na kusababisha chuki na uchochezi wa uasi.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News