Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

UBAGUZI WA MADHEHEBU YA DINI YA KIISLAMU WAPIGWA MARUFUKU BUKOLI GEITA,SHEHE AL-NOOBIY ATAKA WAWE NA UMOJA.

  
KATIBU WA MASJID AL-WAHAB SHEHE AHMED AL-NOOBIY AKIZUNGUMZA NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU KATIKA UFUNGUZI WA MASJID AL-FALAAHI BUKOLI GEITA
 GEITA
Madhehebu ya dini  ya Kiislamu katika kata ya Bukoli mkoani Geita yametakiwa kutokubaguana na kutengana badala yake wawe kitu kimoja katika kuimarisha uislamu na kudumisha umoja katika jamii.

Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Katibu wa Masjid Al-wahab Shehe Ahmed Al-noobiy wakati wa uzinduzi wa Masjid  Al Falaahi uliofanyika katika kata ya Bukoli mkoani Geita.

Al-noobiy amewataka waislamu wa Bukoli kuwa kitu kimoja na kupendana ili kuupeleka uislamu mbele na kuacha tabia ya kujitambulisha kwa dhehebu kwani kitendo hicho kimepelekea maeneo mengi uislamu kukosa nguvu.

Sambamba na hayo Shehe Al-noobiy ameitaka jamii kuondokana na mawazo potofu  kuwa misaada ya misikiti inayojengwa na Jumuiya ya kiislamu ya Isiqaama ya nchini oman inakuwa ya taasisi hiyo na siyo mali ya waislamu wa eneo husika.

Naye mwenyekiti wa Masjid Al-wahab ya Mjini Kahama Mohamed Al-habsy amewataka waislamu kuzitunza nyumba za ibada huku Imamu wa Masjid Al-falaah ya Bukoli Geita Rashid Salum akitoa shukrani kwa niaba ya waislamu wenzake kwa ujenzi wa msikiti huo.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Bukoli Faraji Rajab amewataka wazazi kuendelea kuwasomesha watoto elimu ya dini na elimu ya duniani ili waje kuwa viongozi wa baadaye na kusimamia kikamilifu nyumba za ibada.

MATUKIO KATIKA PICHA:

IMAMU WA MASJID AL-FALAAHI AKISIKILIZA RASHID SALUM AKISIKILIZA KWA MAKINI MAWAIDHA KATIKA UFUNGUZI HUO.

WATOTO WA MADRASA WAKIIMBA NYIMBO ZA KUMSIFU MTUME MOHAMED S.A.W

WAUMINI WA KISLAMU KATIKA KATA YA BUKOLI GEITA WAKIENDELEAKUWASILI KATIKA TUKIO LA UFUNGUZI WA MASJID AL-FALAAHI

MAWAIDHA YAKIENDELEA KATIKA UFUNGUZI HUO.

MWONEKANO WA UBAVUNI WA MASJIDI AL-FALAAHI BUKOLI GEITA.

MASJID AL-FALAAHI ULIOPO BUKOLI MKOANI GEITA.

USTADHI HASSAN SAID AKITOA NENO KATIKA UZINDUZI WA MASJID AL-FALAAHI.

MAMU WA MASJID AL-FALAAHI AKISIKILIZA RASHID SALUM KUSHOTO AKITOA NENO LA SHUKRANI KATIKA TUKIO HILO LA UFUNGUZI WA MASJID.

MWENYEKITI WA MASJID AL-WAHAB YA MJINI KAHAMA MOHAMED AL-HABSY AKITOA WOSIA KUWATAKA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU BUKOLI GEITA KUJITOA KATIKA KUUTUNZA MSIKITI HUO.

DIWANI WA KATA YA BUKOLI FARAJI RAJAB SEIF AKITOA NENO KWA WAISLAMU WALIOFIKA KATIKA UZINDUZI WA MASJID HIYO.

WANAWAKE NA MABINTI WAKIWA KATIKA ENEO LAO LA KUSWALIA NDANI YA MASJID AL-FALAAHI.

MWENYEKITI WA MASJID AL-WAHAB YA MJINI KAHAMA MOHAMED AL-HABSY AKITOA WOSIA KUWATAKA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU BUKOLI GEITA KUJITOA KATIKA KUUTUNZA MSIKITI HUO.

WAUMINI WAKIENDELEA KUSIKILIZA KWA MAKINI WOSIA WA VIONGOZI MBALI MBALI.

MTOTO SALMIN MASOOD AKISOMA QURAN KATIKA UZINDUZI WA MASJID AL-FALAAHI.

WAISLAMU WAKIWA MSIKITINI KATIKA TUKIO LA UFUNGUZI WA MASJID AL-FALAAHI.

ENEO LA VYOO VYA WANAWAKE NA MWONEKANO WA MBELE WA MASJID AL-FALAAHI.

MZEE ABDALLAH ISSA MBARAK AKITOA NENO KWA WAZAZI KUWASOMESHA WATOTO KATIKA ELIMU YA DUNIA NA MADRASA ILI KUWAANDAA KUWA VIONGOZI WAKUBWA BAADAYE.
MABINTI NA WANAWAKE WAKIWA KATIKA ENEO LAO LA KUSWALIA.
BAADA YA SHUGHULI ZOEZI LA KUPATA CHAKULA LIKAFUATIA.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News