Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

MWAKA MMOJA WA DC MURO WILAYA YA ARUMERU KATIKA SEKTA YA ELIMU.


SEKTA YA ELIMU
 Ndugu zangu wana Arumeru kama mtakumbuka nilipoteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Tarehe 28/07/2018 Wilaya yenye Halmashauri mbili, Arusha Dc na Meru Dc zenye jumla ya tarafa 6 na  kata 53 Zenye Majimbo mawili ya Arumeru Mashariki na Magharibi  Moja kati ya kazi niliyoanza nayo ni kuanzisha kampeni ya ujenzi wa madarasa 107 mapya kwa ajili ya shule za sekondari na msingi ujenzi ambao unagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 2  na sasa tumeweza kujenga vyumba vya madarasa 149 badala ya 107

Leo nimeona busara kuwaletea mrejesho wa kampeni hii ambayo imefikisha mwaka sasa kama ifuatavyo;

1. Katika Halmashauri ya Meru Vyumba 35 vya madarasa ya shule za msingi na Sekondari vimekamilika,

Vyumba 42 vya madarasa ya sekondari na msingi vipo kwenye hatua za mwisho kukamilika, pia tumejiongeza kwa kujenga majengo ya Utawala mawili (2)  hatua ya ukamilishaji, pamoja na Maabara mbili (2) za science zipo hatua ya uezekaji.
Pia tumekamilisha ujenzi wa jengo jipya na la kisasa la wadhibiti ubora wa Elimu.

Hivyo katika Halmashauri ya Meru tumeshajenga vyumba na majengo 82

2.Halmashauri ya Arusha

Madarasa yaliyokamilika 34 ambayo yameanza kutumiwa kwa ajili ya sekondari na msingi na yaliyo katika hatua ya mwisho ni madarasa 73 kwa ajili ya shule za msingi na sekondari, katika Halmashauri ya Arusha jumla ya Madarasa 107 yanajengwa katika kampeni hii.

MAFANIKIO YETU

1. Kampeni yetu ya madarasa mpaka sasa inatupa fursa ya kuwa na jumla ya vyumba vya madarasa 149 kutoka malengo ya kujenga vyumba 107, hivyo tumevuka lengo kwa zaidi ya asilimia 100% 

2. Tumeweza kuongeza uandikishwaji

Wilaya imefanikiwa kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na Elimu ya msingi, sasa katika wilaya ya Arumeru wanafunzi wote wanaopaswa kuanza Elimu ya msingi wanaandikishwa kwa asilimia 100%

 3.Ufaulu, wilaya ya Arumeru.

Wilaya imeendelea kuongoza kwa kuwa wilaya ya kwanza Kitaifa kwa ufaulu wa wanafunzi wa sekondari kidato cha sita (form six), na tuko kwenye kumi bora kwa ufaulu kidato cha nne (form four)

SHUKRANI 
Naomba kuchukua fursa hii kumshukuru sana Mhe Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  kwa kutusaidia fedha kwa ajili ya utoaji wa Elimu bure jambo ambalo limetusaidia kuhamasisha wananchi kuchangia ujenzi wa madarasa

Pili Niwashukuru sana Wakurugenzi wa Halmashauri za Meru Ndugu Emanuel Mkongo na Arusha Dc Bi Advera Nbabagoye na mtangulizi wake Mhe Dkt. Charles Wilson Mahera ,
Pia waheshimiwa madiwani kwa kuridhia utoaji wa vifaa na fedha kidogo , niwashukuru sana Ubalozi wa Japan ambao umetusaidia zaidi ya milioni 100, pia niwashukuru wadau wetu wa maendeleo , viongozi wa dini na wananchi ambao wamesimama na sisi katika kipindi hiki cha kuweka msingi wa Maendeleo ya Elimu katika wilaya ya Arumeru

Sisi Arumeru tunaamini katika Mungu ambae anaendelea kutupa nguvu na uwezo wa kufanya yasiyofanyika

Jerry Cornel Muro
Mkuu wa wilaya ya Arumeru 
Arusha
26/11/2019


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News