Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

KIJANA ANUSURIKA KUFA KAHAMA BAADA YA KUPIGWA NA WACHINA WAKIMTUHUMU KUWAIBIA PESA ZA KAMALI.


KAHAMA
Deus Charles (37) katika halmashauri ya mji wa Kahama wilayani Kahama mkoani Shinyanga amenusurika kufa baada ya kupigwa na watu watano wakiwemo raia watatu wa china na watanzania wawili kwa tuhuma za wizi wa fedha kwenye mabonanza.
Akisimulia tukio hilo baada ya kuruhusiwa kutoka hosipitali ya wilaya ya Kahama Deus Charles amesema alitekwa na watu hao Novemba 12 mwaka huu katika eneo la soko la mkulima la zamani wakaanza kumshambulia kwa kumpiga virungu kisha kumbeba kwenye gari na kumpeleka katika pori dogo la Manzese.
Amesema baada ya kufika huko waliendelea kumpiga kisha kumpora kiasi cha fedha cha shilingi 72,000 alizokuwa nazo huku wakiendelea kumpiga baada ya hapo walimtelekeza katika pori hilo hadi alipokuja kuokotwa na jeshi la zima moto na uokoaji na kupelekwa hosipitali.
Deus Charles amesema watu hao hadi kufikia kumpiga wanamtuhumu kuiba fedha katika mabonanza wanayotumia kuchezesha kamari kuwa amekuwa akiyafungua na kuiba fedha kitu ambacho sio kweli kwani baada ya kuacha kufanya kazi na wachina hao aliendelea na kazi zake hivyo wamekuwa wakimhisi kuwaibia.
Kwa upande mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Kahama, George Masasi amesema kijana huyo walimpokea Novemba 13 akiwa katika hali mbaya na waliendelea kumtibu ambapo leo Novemba 19 wamemruhusu kurudi nyumbani lakini ataendelea kuuguza mguu ambao alipigwa hadi kuvunjika ambapo pia alikuwa na majeraha upande wa kichwani na usoni.
Hata hivyo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Richard Abwao amesema ni kweli tukio hilo limetokea la kupigwa kijana huyo na tayari watuhumiwa wamekamatwa na taratibu za kisheria zikikamilika watafikishwa mahakamani.


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News