Header Ads

ZIARA YA TANO YA DC MURO YATUA KWENYE MRADI WA MAJI WA BILIONI 520

ARUMERU
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro amefanya ziara ya tano ya Ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wa bilioni 520, mradi ambao uliwekewa jiwe la msingi na Mhe Rais. Dkt. John Pombe Magufuli

Dc Muro ametembelea maeneo ya vyanzo vya maji yaliyochimbwa visima pamoja na  uwekaji wa miundombinu  ya mabomba ya kusafirishia maji katika maeneo ya Ngaramtoni, Shamba la mbege (seed farm) pamoja na eneo ka kimyaki  ambapo kazi ya kuunga mabomba makubwa inaendelea uku kukiwa na matoleo ya mabomba madogo ya kusambazia maji kwa wananchi 

Katika ziara hiyo  Dc Muro amehakikisha katika utekelezaji wa mradi huo hakuna sehemu umekwama katika wilaya ya Arumeru na Kuwa hakikisha wananchi wa jiji la Arusha pamoja na wilaya ya Arumeru kuwa mradi huo  unakwenda vizuri na utakamilika ndani ya muda uliowekwa na wananchi kupata maji ya uhakika ambapo mradi huo ukikamilika utakuwa na uwezo wa kutoa lita milioni 200 kwa siku.
MKUU WA WILAYA YA ARUMERU AKIKAGUA MRADI WA BOMB LA MAJI.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!