Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

WANANCHI WAMETAKIWA KUJENGA TABIA YA KUSOMA KATIBA ILI KUTAMBUA HAKI ZAO ZA MSINGI KATIKA KULETA MAENDELEO.

 
MKURUGENZI WA SHIRIKA LA UJUZI.ERA DASTAN KAMANZI AKITOA MAFUNZO KWA RADIO ZA KIJAMII NA ASASI ZA KIRAIA.
PWANI
Watanzania wametakiwa kujenga utaratibu wa kusoma katiba ya nchi yao ikiwa ni pamoja na kujua dira ya maendeleo ya Taifa ili kuwawezesha kutoa michango yenye tija katika kulijenga taifa kiuchumi,Kisiasa na Kiutamauni kuanzia ngazi ya Kijiji hadi taifa.

Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa Shirika la Ujuzi.Era Dastan Kamanzi katika mafunzo ya siku mbili kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019 iliyoanza leo Bagamoyo Mkoani Pwani iliyoandaliwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya Policy Forum.

Kamanzi amesema kuwa  wananchi wengi hawana mazoea ya kusoma katiba na kufuatilia maandiko ya Kitaifa hali inayowafanya washindwe kutambua haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na kutoshiriki katika masuala muhimu ya kitaifa ikiwemo kutojiandikisha katika daftari la wapiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Sambamba na hayo Kamanzi amesema kuwa ili mtu awe raia mwema anatakiwa aijue nchi yake na jamii anayoijenga pamoja na kujua Dira ya nchi yake kwa kuzingatia Amani,Uhuru,Haki na Undugu kwa mujibu wa Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.

Kwa upande wake Afisa Programu Uchechemuzi na Ushirikishaji Kutoka Taasisi ya Policy Forum Iman Khatibu amemtaka kila mwananchi nchini kuwa mlezi wa uhuru wake na kuangalia Malengo yaliyowekwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni pamoja na haki ya msingi ya kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Nao baadhi ya washiriki wameishukuru Taasisi ya Policy Forum kuandaa mafunzo hayo kwani yatawasaidia kuleta mabadiliko katika jamii wanazotoka hususan katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Taasisi ya Policy Forum  yameshirikisha  asasi za Kiraia za LHRC,ADLG,HAFOTA,WACOD,TNHCF,BOSEDA,LANGO,TUSHIRIKI,CODEFA,UNGO,TACCEO Pamoja na Radio nne za kijamii ambazo ni  Kahama Fm,Safari Fm,Mashujaa Fm na Nuru Fm ya Mkoani Iringa.

MATUKIO KATIKA PICHA:
DARASA LIKIENDELA KATIKA HOTELI YA STELLA MARIS BAGAMOYO PWANI.

 WASHIRIKI WA MAFUNZO WAKIWA MAKINI KUMSIKILIZA MKUFUNZI DASTAN KAMANZI (HAYUPO PICHANI)


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News