Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

WAISLAMU WILAYANI KAHAMA WATAKIWA KUTUMIA MISIKITI KUDUMISHA AMANI NA KUIMARISHA UPENDO.KAHAMA
Wito umetolewa kwa wa waislamu Wilayani Kahama mkoani Shinyanga kutumia Misikiti katika kuimarisha amani,Upendo,utulivu na ushirikiano pamoja na kutoa elimu watu waache kujichukulia sheria mkononi.

Wito huo umetolewa leo na Shehe mkuu wa Wilaya ya Kahama Omary damka ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Masjid Ummul-mukhtari uliopo Nyasubi eneo la Nyakato ya Magwanji.

Shehe Damka amesema kuwa Misikiti ikitumika vizuri itaimarisha amani na kuondoa uvunjifu wa amani katika jamii ikiwa ni pamoja na kuongeza upendo miongoni mwa wanadamu.

Sambamba na hayo Shehe Damka amewataka madereva wa boda boda na magari kufuata sheria na taratibu za usalama barabarani ili kupunguza ajali ambazo zinapunguza nguvu kazi katika jamii.

Kwa upande wake Mwenyekiti na katibu  wa Masjid Al-wahab ambao ndiyo wamesaidia kupatikana kwa msikiti huo Mohamed Al-habsy na Shehe Ahmed Al-Nuby wamewataka waislamu kuhuheshimu na kuutunza msikiti huo pamoja na kushikamana na kuacha mafarakano.

Awali akisoma risala ya msikiti huo Mohamed Nassoro Mohamed ameishukuru serikali kwa kutoa eneo la Nyakato Magwanji ili kuweza kujengwa msikiti huo kwani waislamu wa eneo hilo walikuwa hawana sehemu ya karibu ya kuabudia.


Jumuiya ya kislamu ya International Istiqaama Community ya nchini Oman imeendelea kutoa misaada ya ujenzi wa misikiti na uchimbaji wa visima katika maeneo mbali mbali nchini  ili kusaidia jamii.

MATUKIO KATIKA PICHA:

SHEHE MKUU WA WILAYA YA KAHAMA OMARY  DAMKA AKIFUNGUA RASMI MSIKITI WA UMMULMUKHTARI 


MWONEKANO WA MSIKITI WA UMMULMUKHTARI ULIOJENGWA  KATIKA ENEO LA NYAKATO NYASUBI ENEO LA MAGWANJI.

 WAISLAMU WAKIWA KATIKA IBADA YA UFUNGUZI WA MSIKITI HUO,ILIYOOANGOZWA NA SHEHE MKUU WA WILAYA YA KAHAMA OMARI DAMKA.

 IBADA IKIENDELEA KATIKA MSIKITI WA UMMULMUKHTARI ENEO LA NYAKATO MAGWANJI.

 DUA MBALI MBALI ZIKIENDELEA KUSOMWA KATIKA UFUNGUZI WA MSIKITI HUO.

 KATIBU WA MSIKITI WA AL-WAHAB KAHAMA AHMED HAROUN ABDURAHMAN AL-NUBY AKIZUNGUMZA KATIKA UZINDUZI WA MSIKITI HUO.

 WAISLAMU WAKISIKILIZA MAWAIDHA YA SHEHE MKUU WA WILAYA YA KAHAMA OMARY DAMKA HAYUPO PICHANI.

 MWENYEKITI WA MASJID AL-WAHAB KAHAMA MOHAMED ISSA HILALY AL-HABSY (KUSHOTO) AKITOA NASAHA ZAKE KWA WAISLAMU WALIOHUDHURIA KATIKA UZINDUZI WA MSIKITI HUO,KULIA NI KATIBU WA MSIKITI AL-WAHAB AHMED HAROUN ABDURAHMAN AL-NUBY

 UFUNGUZI WA MADRASA AMBAYO ITATUMIKA KUWAFUNDISHA WATOTO ILIYOJENGWA KATIKA MSIKITI HUO ENEO LA NYAKATO.


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News