Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

WAANDISHI WA HABARI RADIO ZA JAMII 25 WAPEWA MAFUNZO NAMNA KURIPOTI MAAFA

 WAANDISHI WA HABARI ZA RADIO 25 ZA KIJAMII WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA.

PWANI:
WAANDISHI wa habari kutoka kanda zote nchini ambao wanahudumu katika redio za jamii, wameingia katika mafunzo ya siku 5 mjini hapa kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine.

Katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) washiriki watajifunza namna ya kuripoti maafa na pia mfumo wa kitaifa wa kukabiliana na majanga.

Akizungumza mjini hapa Christophe Legay, Mratibu wa Mradi wa SDC kutoka UNESCO amesema kwamba kutokana na kuongezeka kwa majanga na uelewa duni wa wananchi, UNESCO imeona vyema kufunza wanahabari ili waweze kuelimisha jamii.

Alisema kwamba mafunzo hayo ni ya tatu kwa waandishi wa habari na yamegusa wale ambao hawajawahi kupatiwa mafunzo hayo.

Legay alisema kwamba kutokana na mabadiliko ya tabianchi majanga ya asili yamekuwa yakijitokeza sana na kwa kasi hivyo imeonekana haja ya kuwapatia wananchi mafunzo maalumu ya kukabiliana na majanga hayo ikiwa na pamoja na kujiweka tayari.

"Tunataka wananchi watambue namna ya kukabiliana nayo majanga hayo, ili kusaidia kufikisha taarifa sahihi kwa jamii ambayo wanaitumikia" alisema Legay na kuongeza kuwa wanapowanoa waandishi wamelenga kuwawezesha kuwa na namna bora ya kuandika habari za majanga ili kusaidia kuokoa na kujipanga lisitokee tena.

Alisema kwa sasa wengi wa waandishi namna yao ya kuandika hairidhishi na hivyo kuchochea zaidi hasara badala ya kukabiliana na dhiki hiyo na kuokoa maisha na mali.

Legay alisema watu wakitambua namna ya kusimamia maafa na matumizi ya raslimali na nyenzo za usimamizi hasara kwa mali na watu zitapungua.

Alisema pamoja na majanga ya asili yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi, pia kuna majanga yanayosababishwa na shughuli za binadamu kama vile milipuko ya matanki, ajali mbalimbali ambazo wananchi amekuwa wakijihudumia badala ya kuokoa mali na watu.
Mratibu wa Mradi wa SDC kutoka UNESCO, Christophe Legay akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wakati akifungua mafunzo ya siku 5 kwa waandishi wa redio jamii 25 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.

 Mtaalamu wa Sayansi asilia kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Kevin Robert akizungumza na washiriki wakati akifungua mafunzo ya siku 5 kwa waandishi wa redio jamii 25 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.
 Mratibu wa Asasi ya Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO), Irene Makene akitoa salamu TADIO kwa waandishi 25 wa redio jamii wanaoshiriki mafunzo ya siku 5 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.
 Washiriki kutoka redio za jamii wakichangia maoni wakati wa mafunzo ya siku 5 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.
Baadhi ya ya waandishi 25 wa redio jamii wanaoshiriki mafunzo ya siku 5 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.
Waandishi 25 wa redio jamii wanaoshiriki mafunzo ya siku 5 ya kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine yaliyoandaliwa na UNESCO chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) yanayofanyika katika hoteli ya Millenium Sea Breeze mjini Bagamoyo.


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News