Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

SERIKALI IMESHAURIWA KUWA NA SERA YA USIMAMIZI WA MATUMIZI BORA YA ARDHI ILI KUKABILIANA NA MAFURIKO.


PWANI
Katika kukabiliana na majanga ya mafuriko  kwenye maeneo mbalimbali nchini, serikali imeshauriwa kuwa na  sera ya usimamizi wa  matumizi  bora ya ardhi.

Hayo yamebainishwa mjini Bagamoyo mkoani Pwani  na  Mtaalamu wa masuala ya Sayansi Asilia kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) CALVINE ROBART wakati akizungumza na waandishi wa habari  wa redio za kijamii nchini wanaohuduhudhuria  mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuandika na kuandaa vipindi vya majanga.

Amesema  maeneo mengi nchini yanayoathiriwa na mafuriko ni yale ambayo  yameshindwa kutekeleza  matumizi bora ya ardhi kwa kufanya  ujenzi wa makazi holela pamoja na watu kujenga katika maeneo ya mabonde   bila kujali madhara yanayoweza kujitokeza.

Hata hivyo ROBART ameongeza kuwa  serikali inauwezo  wa kutekeleza sheria ya kuwahamisha  kwa nguvu wananchi  waliopo kwenye maeneo yanaayoonekana kuwa katika  hatari ya kukumbwa na  mafuriko kwa kuwa  hakuna sheria inayoruhusu  kuweka makazi kwenye maeneo yenye vyanzo vya maji.

Majanga  kama mafuriko na Ukame kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakisababishwa na shughuli za kibinadamu ikiwamo  ujenzi wa makazi holela, na ukataji wa miti  huku pia  yakisababishwa na   mabadiliko ya tabia ya  nchini.

Kwa Mujibu wa Sheria ya usimamizi wa rasilimali za maji,  na  mazingira   kifungu cha 57 kifungu kidogo cha 1, namba 20  ya mwaka 2004 inaelekeza kusifanyike shughuli zozote  za kibinadamu  ndani ya mita 60 kutoka  chanzo cha maji.


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News