Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

IMANI ZA KISHIRIKINA ZAHUSISHWA MECHI YA BALELE NA UJENZI FC KAHAMA,MVUA YA UPEPO YASAMBARATISHA MCHEZO.


KAHAMA
Mchezo wa kuwania kuingia Fainali ya Kahama Fm Bonanza kati ya Balele Fc na Ujenzi Fc umeshindwa kuendelea leo Katika Uwanja wa Halmashaui baada ya mvua kubwa ya Upepo mkali kunyesha katika kipindi cha pili cha mchezo huo.

Katika mchezo huo Balele walifanikiwa kupata gori la kwanza katika kipindi cha kwanza kupitia mchezaji wake anayefahamika kwa jina la Lukaku.
Kipindi cha pili cha mchezo huo wingu zito lilitanda na baadaye mvua kubwa kunyesha hali iliyopelekea Mshika kipenga Juma Sudi Jumeju kusitisha mchezo huo baada ya mvua kuwa kubwa.

Leo Balele Fc ilitakiwa kupata mabao mawili ili kufuzu kuingia Fainali ya Kahama Fm Bonanza ambapo katika mchezo wa kwanza Ujenzi Fc iliifunga Balele bao moja kwa bila.

Hivyo kutokana na matokeo hayo Timu zote ziko sawa kimatokeo na makubaliano kati ya waaandaji wa Bonanza hilo na Viongozi wa Timu ni kwamba mchezo wa leo umefutwa na na mechi hiyo itarudiwa siku ya Jumatano.

Mratibu wa Mashindano hayo Sebastian Komaa amesema kuwa amezungumzana viongozi wa Timu zote na wamekubaliana mchezo huo kurudiwa siku ya Jumatano.

Nao baadhi ya mashabiki wamehusisha mvua hiyo na imani za kishirikiana na kwamba huenda timu moja wapo iliona dalili za kuzidiwa katika mchezo huo.

Kwa upande wake Meneja wa Timu ya Ujenzi Fc Joseph Nalimi amesema kuwa kuwa wao hawaamini katika ushirikina na kwamna mvua hiyo ni mvua kama zilivyo mvua zingine na kwamba wanaenda kujiandaa kwa ajili ya mchezo ujao.

Naye msemaji wa Balele Fc bwana Benjamini amesema kuwa mvua hiyo ni mvua ya kawaida na kwamba wao wanaamini katika uwezo wa wachezaji na kwamba wako tayari kusubiri mchezo ujao.


Mashindano ya Kahama Fm Bonanza yamefika katika hatua ya Nusu fainali ambapo timu nne zinapigania kuingia katika Fainali hiyo ambao ni Balele Fc,Ujenzi Fc,Ambasador Sports Academy na Vijana Chato kutoka mkaoni Geita.

MATUKIO KATIKA PICHA:
SEHEMU YA JUKWAA LA VIONGOZI WA TIMU IKIWA IMEHARIBIKA BAADA YA MVUA KUNYESHA LEO.

MWONEKANO WA UWANJA BAADA YA MVUA KUBWA KUNYESHA LEO.

HALI YA UWANJA ILIVYOKUWA MARA BAADA YA MVUA KUNYESHA KAHAMA LEO.
WACHEZAJI NA MASHABIKI WAKIREJEA UWANJANI MARA BAADA YA MVUA KUPUNGUA.

WAAMUZI WAKIKAGUA UWANJA KAMA UNAWEZA KUENDELEA KATIKA MCHEZO HUO.

WACHEZAJI WAKIREJEA UWANJANI BAADA YA MVUA KUKATIKA,ILA MCHEZO ULISHINDWA KUENDELEA BAADA YA UWANJA KUJAA MAJI.

KUFA KUFAANA JAMAA ALIANZA KUVUSHA WATU KWA SHILINGI ELFU ELFU MBILI KUTOKA UPANDE MMOJA KWENDA UPANDE MWINGINE.

WAFANYAKAZI WA KAHAMA FM WAKINUSURU VIFAA VYAO VYA MZIKI MARA BAADA YA MVUA KUNYESHA.

MRATIBU WA KAHAMA FM BONANZA SEBASTIAN KOMAA AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI KUHUSU NAMNA GANI MCHEZO HUO UTAKAVYORUDIWA.

MAJUKWAA YAKIWA MEUPE MARA BAADA YA MASHABIKI KUTAWANYIKA KUKIMBIA MVUA.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News