Header Ads

MBARONI KWA KUJIANDIKISHA MARA 2 KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

Mkazi wa Kasanga Manispaa ya Morogoro, Ngeze Mwagilo (29) anatuhumiwa kujiandikisha mara mbili katika Daftari la Wapiga Kura kwenye vituo viwili tofauti ndani ya Manispaa ya Morogoro

Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Wilbroad Mutafungwa amesema mtu huyo alikamatwa baada ya Polisi kupata taarifa na kumfuatilia Mtuhumiwa wakati wa shughuli ya uandikishaji

Amesema, mtuhumiwa huyo anadaiwa kujiandikisha katika Kituo cha Kasanga Kata ya Mindu na baadaye kwenda kujiandikisha katika Kituo cha Kiwanja cha Ndege Kata ya Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro

Aidha, Kamanda Mutafungwa amebainisha kuwa Mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa na atafikishwa Mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika ili sheria ichukue mkondo wake

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!