Header Ads

ASASI ZA KIRAIA ZATAKIWA KUFUATILIA AHADI ZA WAGOMBEA WAKATI WA KAMPENI.


MKURUGENZI WA KAMPUNI YA UJUZI.ERA DASTAN KAMANZI AKITOA MAFUNZO KWA ASASI ZA KIRAIA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA HOTEL YA STELLA MARIS BAGAMOYO MKAONI PWANI.

PWANI
Asasi za kiraia zimetakiwa kufuatilia ahadi za wagombea tangu kipindi cha kampeni ili kuweka taarifa na kumbukumbu sahihi na kuacha tabia ya kufanya ufuatiliaji wa utekekelezaji wa ahadi pasipo kuwa na kumbukumbu za  nini alihaidi kabla ya uchaguzi.

Wito huo umetolewa leo Bagamoyo mkoani Pwani  na Mkurugenzi wa kampuni ya Ujuzi.Era Dastan Kamanzi katika siku ya pili ya mafunzo kwa waandishi wa habari za radio za kijamii na asasi zisizo za kiserikali yaliyoandaliwa na Taasisi ya Policy Forum.

Kamanzi amesema kuwa asasi nyingi za kiraia zimekuwa na mfumo wa kufuatilia mambo nusu nusu hali inayowagombanisha na viongozi wa kisiasa wakati wa uchaguzi kwa kuhoji ahadi za miaka ya nyumba pasipokuwa na kumbukumbu hizo.

Ameongeza kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa ni vyema asasi zikazunguka kuweka kumbukumbu watakazotoa wagombea katika mitaa na vijiji ili kuzitumia pindi wanapofanya ufuatiliaji.
 AFISA MIPANGO WA TAASISI YA TACCEO WAKILI JOSEPH OLESHANGAY

Kwa upande wake afisa mipango wa Taasisi ya TACCEO wakili Joseph Oleshangay ametoa wito kwa Asasi za kirai na vyombo vya habari kutekeleza majuku yao kwa kufuata Sheria za nchi na kanuni za uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Policy Forum yaliyoshirikisha washiriki 21 kutoka asasi za kiraia na Radio nne za kijamii yamehitimishwa leo Bagamoyo mkoani Pwani. 
No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!