Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

AS ROMA YAWA TIMU YA KWANZA YA ULAYA KUFUNGUA TWITTER YA KISWAHILI

Timu ya soka ya 'As Roma' ya nchini Italia imekuwa klabu kubwa ya kwanza barani Ulaya kuanzisha ukurasa wake katika mtandao wa Twitter kwa lugha ya Kiswahili.

Ukurasa wa klabu hiyo mashuhuri nchini Italia na barani Ulaya ambayo ilianzishwa mwaka 1927 utakuwa ukiandika habari zake kwa lugha adhimu ya Kiswahili.

Ukurasa huo wa lugha ya Kiswahili ulizinduliwa rasmi jana, na inaaminika lengo kuu la 'As Roma' ni kuwafikia mamilion ya watu wanatumia lugha ya Kiswahili katika eneo la Afrika Mashariki na maeneo mengine duniani.

Baada ya kuzinduliwa ukurasa huo, wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili katika maeneo mbalimbali wameonekana wakipongeza hatua hiyo na kuanza kutoa maoni yao katika ukurasa huo. 

Msimamizii wa ukurasa huo ameandika haya baada ya kuzinduliwa ukurasa huu: Ahsante kwa upendo na ushirikiano ambao mmetuonyesha tangu tumezindua ukurasa huu rasmi. Ni dhahir kwamba, kwa pamoja tutaendelea kushirikiana na kufurahia pamoja hapa hapa kwa lugha ya Kiswahili.
Itakumbukwa kuwa katika mkutano wake mwezi uliopita huko jijini Dar es Salaam Tanzania Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ilipitisha pendekezo kuwa Kiswahili kianze kutumika kama lugha ya nne katika jumuiya hiyo.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News