Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

AFARIKI DUNIA KWA KUPIGWA SHOTI YA UMEME KAHAMA,


KAHAMA
Na Salvatory Ntandu
Mkazi wa Mtaa wa Igalilimi katika Halmashauri ya Mji wa  kahama mkoani Shinyanga,aliyefamika kwa jina Juma Matondo mwenye umri unaokadiriwa kuwa ni miaka 20-22  amefariki dunia baada ya kupigwa na shoti ya umeme wakati akianika nguo kwenye kamba ya nyumba yao iliyosababishwa na waya wa umeme kukatika na kuangukia juu ya paa la nyumba yao.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema mafundi wa Tanesco kahama ndio wakulaumiwa katika  kifo cha Mtu huyo kwani walifanya matengenezao ya umeme kwa uzembe kwa kuacha nyaya zenye umeme zikining’inia na kugusa bati zikiwa na umeme.

ESTA MUSA ni mmliki wa nyumba hiyo ambayo Marehemu Juma alikuwa akifanya kazi amesema jana alitoa taarifa za hitilafu ya umeme katika nyumba yake lakini Mafundi wa Tanesco walipokuja walifanya kazi na kuacha nyaya zikiwa zinagusa bati jambo lilisababisha umeme kuenea katika paa la nyumba yake.

Naye Diwani wa kata ya Kahama Mjini, Hamidu Juma Kapama  amesema baada ya kutokea kwa tukio hilo wamekaa na Meneje wa Tanesco kahama Mhandisi King Fokanya na kukubaliana ofisi yake kulipia gharama zote za msiba pamoja na kuusafirisha mwili wa marehemu kwenda mkoani Kigoma kwaajili ya Mazishi.

Kijukuu Blog imefika katika ofisi ya  meneja wa Tanesco wilaya ya kahama King Fokanya ili kujua undani zaidi wa tukio hilo lakini amekataa kuzungumza kwa madai kuwa yeye si msemaji wa Shirika hilo na tayari ameshatuma taarifa mkoani.

Mganga mfawidhi wa hopitali ya Halamshauri ya Mji wa Kahama George Masasi amekiri kupokea mwili wa Juma ambaye amefariki kwa kupigwa na shoti ya Umeme katika eneo la Igalilimi.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News