Header Ads

WAZIRI MWINYI AWAAGIZA SUMA JKT KUFANYA UTAFITI WA UVUNAJI WA MAJI YA MVUA SHINYANGA


KAHAMA
Na Ndalike Sonda (Kijukuu Blog) 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. HUSSEIN MWINYI ameagiza Uongozi wa Shirika la  SUMA JKT kanda ya Ziwa kupeleka wataalam mkoani Shinyanga  kwaajili ya kufanya utafti  wa kilimo cha umwagiliaji na uvunaji wa maji ya mvua ili kuanzisha miradi hiyo mkoani humo.

Dokta MWINYI ametoa kauli hiyo mjini Kahama  baada ya kupokea ombi  hilo kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga ZAINAB TELACK kwenye  ziara ya kukagua miradi  ya ujenzi inayotekelezwa na Suma JKT.

Dokta MWINYI amesema Suma JKT imekuwa ikishiriki katika miradi  ya sekta mbalimbali hivyo ni vyema  suala hilo likafanyiwa kazi ili kuendelea kutekeleza adhma ya serikali ya kuwa na  uchumi wa kati.
  
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa shirika la  Suma JKT, KANALI RAJAB  MABELE amesema  ombi la Mkuu wa mkoa wa Shinyanga wamelichukua kama fursa kwao na kwamba  wataalamu hao wafika mkoani humo siku chache zijazo.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga TELACK amesema kama  Suma JKT italeta mradi wa uvuanaji maji ya mvua  ni wazi kwamba wananchi wa mkoa huo wataweza kujishughulisha na kilimo cha umwagiliaji na hivyo kujipatia kipato.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!