Header Ads

WAZIRI AAGIZA WASHEREHESHAJI WA HARUSI WASIOKUWA NA VITAMBULISHO WAKAMATWE KAGERA.

Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera
Waziri  wa Habari sanaa utamaduni na michezo Dokta Harrison Mwakyembe ametoa agizo la kuwasaka  kubaini na kuwakamata washereheshaji wa  harusi maarufu kama mc mkoani Kagera ambao hawana vitambulisho vya kazi hiyo na kuwa atakayebainika atachukuliwa sheria kali ikiwemo harusi hiyo kusimama wakati huo.
 
 Waziri Mwakyembe  ametoa kauli hiyo August 30 Mwaka huu wakati akiwa mkoani Kagera katika mkutano na  wadau wa sekta ya habari utamaduni sanaa na michezo uliofanyika katika ukumbi wa mkoa uliopo Bukoba manispaa mkoani hapa.
 
Waziri Mwakyembe amesema kuwa tayari serikali imeishaweka utaratibu wa kila mfanya  biashara kuwa na kitambulisho na kudai kuwa utaratibu huo unajulikana  nchi nzima.
 
 Ametaja kuwa  kitendo cha  baadhi ya washereheshaji kunyonya jasho la ambao tayari wamelipia vitambulisho vya kuwatambua katika kazi hiyo ni kosa kisheria.
 
Waziri huyo Amesema ni jambo la kusikitisha na kutoa agizo la Wakaguzi kufanya  msako mkali ili kubaini washereheshaji ambao hawajasajiliwa na kuwa wakibainika watachukuliwa sheria kali ikiwemo harusi hiyo kusimamishwa wakati huo.  
 
Amesema  sambamba na kuwachukulia sheria kali watatozwa Faini itakayo ingizwa  katika mfuko wa wasanii ili kuinua tasnia ya utamaduni na sanaa.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!