Header Ads

WAZEE KAHAMA WAMEWATAKA VIJANA KUWA NA MOYO WA KUWASAIDIA WAZEE WENYE UHITAJI.Na Ndalike Sonda (Kijukuu Blog)
KAHAMA

Baraza la wazee katika  halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga limeitaka jamii  hasa kundi la  vijana kuwa na moyo wa kuwasaidia  wazee wenye uhitaji ili waweze kuishi maisha yasiyotegemezi.

Wito huo umetolewa leo mjini Kahama na Mwenyekiti wa baraza hilo WILLFRED BIRAGO wakati akizungumza na waamini wa kanisa  katolika  la Mtakaifu Karoli Lwanga  ikiwa ni mwendelezo wa baraza hilo wa kutoa elimu ya wazee kwenye makanisa na misikiti mbalimbali  ndani ya halmashauri  hiyo.

Amesema  wazee wengi hasa  waliopo vijijini wameshindwa kuisha maisha bora kutokana na  kutelekezwa na watoto wao  na kwamba jambo hilo linazidi kuwaumiza wazee kwa kuwa hawana  nguvu ya kujipatia kipato.

BIRAGO amesema wazee wanahitaji kusaidiwa katika Nyanja mbalimbali ikiwamo  Afya ambapo ameitaka jamii kuwasaidia wazee kuwakatia bima ya afya  ya jamii (CHF) iliyoboreshwa ambayo inapatikana kwa kila watu sita ni shilingi 30,000  kwa mwaka mmoja.

Paroko wa Parokia hiyo  Padri SALVATORE QUERRERA amelipongeza  baraza la wazee kwa juhudi za kutoa elimu kwa wananchi ili kuwa  na uelewa wa namna ya kuwasaidia wazee na kuwataka waumini wa kanisa hilo kuwa na Moyo wa kuwasaidia watu wenye uhitaji.

Baraza  la  wazee katika halmashauri ya Mji wa Kahama  kwa kushirikiana na Chama cha  wanawake wataalamu wa  Mazingira na Kilimo Tanzania TAWLAE  wanaendelea kutoa elimu   ya kuwatambua wazee katika ushirikishwaji wa masuala mbalimbali ikiwamo katika kutoa maamuzi katika jamii na halmashauri.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!