Header Ads

WATU WAWILI WAFARIKI KATIKA VURUGU MPYA NCHINI AFRIKA KUSINI

Watu wawili wameripotiwa kufariki hapo jana baada ya kuzuka kwa vurugu mpya nchini Afrika Kusini.

Vurugu hizo zilizuka baada ya hotuba ya mwanasiasa Mangosuthu Buthelezi mjini Johannesburg, dhidi ya vitendo vya chuki dhidi ya wageni.

Watu 10, wakiwemo wageni wawili, waliuawa mjini humo juma lililopita, baada ya makundi ya watu kuvamia biashara zinazofanywa na raia wa kigeni.

Vurumai hizo zimesababisha mvutano wa kidiplomasia na nchi nyingine za kiafrika, hasa Nigeria, huku raia 640 wa Nigeria nchini Afrika kusini wakirudi nyumbani.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!