Header Ads

WANANCHI KAHAMA WAREJEA KUTIBIWA KATIKA ZAHANATI WALIYOIKATAA BAADA YA MTUMISHI ALIYEKUWA ANATUHUMIWA KUWATAKA KIMAPENZI WAGONJWA KUSIMAMISHWA KAZI.


Na Ndalike Sonda (Kijukuu Blog)
KAHAMA
Baadhi ya wananchi wa Kijiji Cha Sangilwa Kata ya mondo katika halmashauri ya Mji wa Kahama wamesema wameanza kuitumia zahanati ya  Kijiji hicho kupata  huduma ya matibabu baada ya halmashauri hiyo kumsismamisha kazi  mtumishi  mmoja aliyekuwa anatuhumiwa kuwataka kimapenzi wagonjwa wanawake wanaokwenda kutibiwa.

Wakizungumza na Kijukuu Blog,  wananchi hao wamesema kwa sasa wamekuwa na imani kubwa na huduma zainazotolewa kutokana  na  serikali kusililiza kero iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa eneo hilo, dhidi ya mtumishi huyo.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha SANGILWA VICENT MAYALA amesema wananchi kwa sasa hawazungumzii jambo hilo baada ya halmashauri kumsimamisha kazi mtumishi huyo, huku Muuguzi wa Zahanati hiyo  JACKLINE JOHN akiwataka wananchi kuitumia Zahanati hiyo.

Hivi karibuni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Kahama ANDERSON MUSUMBA aliliambia baraza la madiwani kuwa  wamemsimamisha kazi Mtumishi wa zahanati hiyo aliyemtaka kwa jina moja la RAMA kwa tuhuma za kuwataka kimapenzi wanawake wanaokwenda kutibuwa katika zahanati hiyo.

MUSUMBA alisema hiyo si mara ya kwanza kwa RAMA kuwa na tuhuma kama hiyo ambapo mara ya kwanza alituhumiwa katika Kituo cha Afya Mwendakulima na akahamishiwa katika zahanati ya Sangilwa.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!