Header Ads

WAKAZI KAHAMA WAPONGEZA HATUA YA RAIS MAGUFULI KUKUTANA NA WATENDAJI WA KATA.


RAIS MAGUFULI AKIZUNGUMZA NA WATENDAJI WA KATA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

KAHAMA
Baadhi ya wananchi  wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametoa pongeza kwa Rais JOHN MAGUFULI kwa hatua ya kuwaita maafisa watendaji wa kata nchini ili kuzungmza nao  mausuala ya maendeleo.
Wakizungumza leo mjini Kahama na Kijukuu Blog,  SALUM MUSA na SUZANA  EMANUEL wamesema     kutokana  na  kikao hicho, wananachi wanategemea kuona mabadiliko chanya katika ngazi ya Kata kwa kuwa  Rais MAGUFULI amejaribu kuwafafanulia namna ya  kusimamia   miradi ya maendeleo kwenye kata zao.
Wamesema mategemeo makubwa ya wananchi ni kuja kuona maofisa Watendaji hao, wanakuwa mstari wa mbele katika kusimamia na kuhamasisha  wananchi kuibua na kuitekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kufanya kazi bila woga wowote dhidi ya  viongozi wa ngazi za juu.
Naye  Mzee PAUL NTELYA amewataka Maofisa watendaji  hao kuwa na busara  ya hali ya juu katika utekelezaji wao wa majukumu  ili kuondoa mgongano baina  yao na viongozi wenzao  wa ngazi ya juu.

Jana Rais MAGUFULI amefanya kikao na maofisa Watendaji wa Kata nchini, Ikulu jijini Dar es salaam, ambapo pamoja na mambo mengine amewataka maofisa watendaji hao kubeba kero za wananchi na kuzitatua badala ya kusubiri ziara za viongozi wa kitaifa.


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!