Header Ads

UTUMISHI FC YA USHETU KAHAMA YATINGA ROBO FAINALI KAHAMA FM SPORTS BONANZA.


KIKOSI CHA TIMU YA UTUMISHI FM


KAHAMA
Timu ya Utumishi Fc inayotoka halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama mkoani Shinyanga,Imekuwa timu ya Kwanza kutinga Robo fainali ya Kahama Fm Sports Bonanza 2019.

Timu hiyo inayoundwa na maafisa wa Serikali kutoka Halmashauri  hiyo imetinga Robo fainali baada ya kuichapa Simba motto ya Lowa bao moja kwa Bila.

Akiongea na Kijukuu Blog mara baada ya Mchezo huo kukamilika Kapteni wa timu hiyo Rashid Kilingamoyo amesema kuwa siri ya ushindi wao ni Umoja na kuzingatia mazoezi na kwamba ushindi wa leo ni salamu kwa timu zingine ambazo zinashiriki michuano hiyo.

Kwa upande wake Kocha wa Timu ya Simba motto amesema kuwa wapinzani waliweza kutumia vizuri mapungufu yao ndiyo mana wamewafunga.

Gori la Utumishi Fc liliwekwa nyavuni na Teves Lukui katika kipindi cha pili baada ya kutokea piga nikupige katika gori la Timu ya Simba motto Fc.

SHANGWE BAADA YA USHINDI


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!