Header Ads

UNESCO YAZITAKA RADIO ZA JAMII KUTUMIA DATA SAHIHI KATIKA UANDAAJI WA HABARI NA VIPINDI .

 DODOMA

Shirika la kimataifa linaloshughulika na maswala ya elimu,sayansi na utamaduni UNESCO,limeendesha mafunzo  ya Utafiti wa Wasikilizaji (Audience Survey) kwa Redio za Jamii Tanzania ambayo  yameanza leo Jijini Dodoma.

Akizungumza na Washiriki wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo hayo Afisa Ufuatiliaji na Jinsia kutoka UNESCO Bw Marko Shekalaghe amesema kuwa lengo la Mafunzo hayo ni kuziwezesha Redio za Jamii kufanya tafiti na kutumia data sahihi katika uandaaji wa Vipindi vya Redio.

Aidha Shekalaghe amesema mafunzo haya ni muhimu sana kwa faida ya  radio zetu,kwani tafiti hizo zitasaidia Redio za Jamii kutambua Wasikilizaji wao, Mfumo wa Maisha yao, Mahitaji na Changamoto zinazowakabili.

Kwa upande wake  Mratibu wa mtandao wa radio  za Jamii Tanzania (TADIO) Bi Irene Makene amewataka Washiriki wa Mafunzo hayo kutumia muda wa Mafunzo hayo kuwasikiliza wakufunzi ili waweze kwenda kutumia vyema watakachojifunza kwa manufaa yao na ya Vituo vyao.

Mafunzo hayo ya Siku tano yameandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni(UNESCO). Jumla ya washiriki 26 kutoka Radio za kijamii Tanzania Bara na Visiwani ambao ni wanachama wa TADIO pamoja na sekretarieti ya TADIO wanashiriki mafunzo hayo .


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!