Header Ads

UKWELI KUHUSU WAGANGA WA JADI KUKUTANA BWALO LA POLISI KAHAMA.


KAHAMA
Waganga wa tiba asili wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuwa na ushirikiano katika kuwafichua  waganga matapeli wanaotumia taaluma hiyo vibaya na kuwapeleka katika vyombo vya dola ili ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Kauli hiyo imetolewa na katibu taifa wa Umoja wa Waganga na wakunga wa tiba asili Tanzania(UWAWATA) LUKAS MLIPU katika ziara yake wilayani humo kwa lengo la kutoa elimu kwa waganga dhidi ya kuendesha shughuli zao kwa udanganyifu.

Kwa upande wake, mkuu wa polisi wilayani Kahama LUTUSIO MWAKYUSA amesema waganga wa tiba asili wametakiwa kushirikiana na jeshi la polisi kwa kuwafichua waganga matapeli na kuwataka kuwa waaminifu wanapotibu wagonjwa na kuacha tamaa.

Nao waganga wa tiba asili wilayani humo wakizungumza na kahama fm kwa nyakati tofauti wameshukuru kupatiwa elimu hiyo ili kuwapa na wenzao ambao wapo huko vijijini ili kuepukana na waganga matapeli wanotumia taaluma hiyo kwa kuwadanganya wagongwa.

Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na wakunga wa tiba asili Tanzania(UWAWATA) wilayani kahama, KULWA SAIDI amesema lengo la kikao hicho ni kuzindua kampeni ya kuwapatia elimu elekezi wanganga wilayani humo ili kusaidia jamii kuwatambua baadhi ya waganga matapeli.


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!