Header Ads

TUMBAKU ZILIZOZALISHWA NJE YA MAKISIO WILAYANI KAHAMA SASA KUNUNULIWA.


MKUU WA WILAYA  YA KAHAMA ANAMRINGI MACHA
KAHAMA
Na Ndalike Sonda
Serikali wilayani Kahama mkoani Shinyanga imesema kuwa imefanya ushawishi kwa  kampuni za ununuzi wa zao la tumbaku ili kununua  tumbaku iliyozalishwa nje ya mkataba  katika msimu wa tumbaku 2018/2019.

Mkuu wa wilaya  ya Kahama ANAMRINGI MACHA ameiambia Kijukuu Blog  kuwa  takriban kilo milioni 2.4 za tumbaku zimezailishwa na wakulima nje ya mkataba baina ya kampuni za ununuzi wa zao hilo na wakulima.

Aidha katika kukabiliana na changamoto hiyo, MACHA amewataka wakulima wa tumbaku kulima  na kuzalisha zao hilo kwa kiwango ambacho kipo katika mkataba.

Kwa upande wa zao la Pamba,  MACHA amesema zaidi ya Kilogram milioni  2.6 kati  ya miloni 4.7 zilizolimwa wilayani Kahama zimenunuliwa  na  kampuni za ununuzi na wakulima wameshalipwa  huku Kasi ya ununuzi imeongezeka ambapo hadi kufikia mwisho wa msimu, pamba yote itakuwa imenunuliwa.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!