Header Ads

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AFYA YA ASKOFU MKUU WA JIMBO KATOLIKI DAR ES SALAAM YUDA RUWAICHI BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam nchini Tanzania, Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa'ichi amefanyiwa upasuaji wa dharura katika Taasisi ya mifupa (MOI).

Taarifa iliyotolewa na leo Jumanne Septemba 10, 2019 na Kitengo cha Mawasiliamo MOI inaeleza Askofu Ruwa'ichi alipokelewa hospitalini hapo jana Jumatatu saa 5 usiku akitokea Hospitali ya KCMC, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Baada ya kupokelewa hospitalini hapo, wataalamu wa MOI walimfanyia uchunguzi na vipimo na kubaini alihitaji upasuaji wa dharura
.

tangazo

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!