Header Ads

SWALI LA KWANZA ALILOULIZA MRITHI WA LISSU BUNGENI

Mbunge wa Singida Mashariki (CCM), Miraji Mtaturu leo ameuliza swali lake la kwanza bungeni baada ya kuapishwa.

Spika, Job Ndugai baada ya kumuona alisema, “Nimekuona Mbunge Mtaturu naomba uulize swali la nyongeza.”

Mtaturu amesema , “Ninaomba mheshimiwa Waziri anihakikishie kwamba kupitia tathmini iliyofanyika na ipo wizarani, tunahitaji jumla ya Sh2 bilioni tuweze kuwatengenezea miundombinu ya maji wananchi wa Singida Mashariki.”

Akijibu swali hilo Aweso amesema, “Awali ya yote kwanza nimpongeze mbunge, kwanza namfahamu vizuri alikuwa mkuu wa wilaya lakini nataka niwahakikishie wana Singida Mashariki hili ni jembe alitumie vizuri.”

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!