Header Ads

SUMA JKT WATAKIWA KUKAMILISHA UJENZI WA HOSPITALI YA MJI WA KAHAMA KWA MUJIBU WA MIKATABA.


Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA-JKT) kanda ya ziwa limetakiwa kuhakikisha linakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Halimashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga kwa mujibu wa  mkataba.

Agizo hilo limetolewa leo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk HUSSEIN MWINYI alipotembelea Hospitali hiyo kukagua maendeleo ya ujenzi utakaogharimu  shilingi bilioni nne nukta mbili kwa lengo la kupanua maeneo ya kutolea huduma kwa wananchi.

Waziri MWINYI amesema baada ya kupokea changamoto mbalimbali za ujenzi huo amesema atahakikisha anazitatua mapema huku akimtaka meneja suma jkt kanda ya ziwa kuhakikisha anakamilisha kwa wakati ujenzi huo.
   
Kwa upande wake, kaimu meneja suma jkt kanda ya ziwa Kepteni, FABIAN BUBERWA amesema endapo baadhi ya vikwazo ikiwemo michoro ya jengo vitatatuliwa watahakikisha wanakamilisha ujenzi huo mwanzoni mwa mwezi february mwakani.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!