Header Ads

SIASA YADAIWA KUKWAMISHA USAILI WA VIJANA KUJIUNGA CHUO CHA VETA VCT


Na Timothy Itembe Mara.

Makamu mkuu wa Chuo cha Tarime Vocational Traning Center (TVCT),Erick Owino ametaja siasa kuwa ni moja ya changamoto inayokwamisha mpango wa vijana kuandikishwa ili kujiunga na chuo hicho kwaajili ya kupata mafunzo ya kozi mbambali ya ufundi.

Akiongea jana kwenye mkutano wa Umoja wa Vijana wa Chama cha mapinduzi UVCCM uliokalia katika ukumbi wa Mwera Vision alisema kuwa moja ya changamoto wanayokumbana nayo katika mpango huo  ni pale ammbapo wanasiasa wanapita na kuwaeleza vijana kuwa mpango huo umefadhiliwa na Chama cha Mapinduzi na vijana kusita kuchukua Fomu za kujiunga.

"Mpango ni mkakati wa miaka mitano ambao  unaolenga  kutoa mafunzo mbalimbali ya ufundi stadi kwa vijana wote wanaozunguka halmashauri ya Mji wa Tarime ndani ya kata nane ambao wamemaliza darasa la saba na waliohitimu shule ya Sekondari lakini hawakubahatika kufauli ili kuendelea na masomo ya juu kwa hali hiyo Chuo kimekuja na mpango wa kuwakomboa vijana ila chuo kinakabiliwa na changamoto kubwa ya baadhi ya wanasiasa  kupita na kukwamisha zoezi hili kwa madai kuwa mpango huo umefadhiliwa na Chama cha mapinduzi jambo ambalo si kweli"alisema Owino.

Owino aliendelea kusema kuwa mpango huo umelenga kuwakomboa vijana wa halmashauri ya mji wa Tarimje hatimaye mpango utahamia na kuwashirikisha vijana wote wa Wilaya nzima ya Tarime lengo likiwa ni vijana hao kupata ujuzi wa fani mbalimbali na kuondokana na kuwa tegemezi kwa jamii.

Kwa upande wake Hezeboni Peter Mwera ambaye ni mkurugenzi wa Mwera Vision alisema kuwa mpango huo ni kuunga juhudi za Rais awamu ya Tano John Pombe Magufuli ya kutoa elimu Bure kwa Shule za Sekondari na Msingi  hapa nchini na Chuo kimekuja na mpango wa kuwakomboa vijana kwasbabu waliokosa frusa ya kuendelea ni wemngi na wanabaki mitaani wakirandaranda hovyo.

Peter aliongeza kusema kuwa kwa sasa chuo chake kinatoa mafunzo ya Udereva Class AB na D mafunzo ambayo yanachukua  wiki Sita na kozi zote ni bure hazilipiwi chochote ambayo yanajumuisha vijana wanaotokana na halmashauri ya Miji wa Tarime pamopja na Kozi ya ufundi Cherehani ikiwemo mafunzo ya Kopyuta ambapo mkurugenzi huyo alitumia nafasi hiyo kuwaomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuunga juhudi za Rais katika kutoa elimu Bure.

Peter alimaliza kwa kusema kuwa Chuo chake kinakabiliwa na uhaba wa vifaa na matirio mbalimbali kwaajili ya kujifunzia ikizingatiwa kuwa mafunzo hayo wanayatoa bure na hawalipwi chochote kinachotakiwa ni mwanachuo kuchangia garama za Tsheti pamoja na Sare za chuo.

Naye katibu wa Umopja wa vijana wa Chama cha mapinduzi UVCCM Wilaya Tarime Newton Mongi alitumia nafasi hiyo kuwaomba vijana wa Chama cha mapinduzi kuondoa tofauti zilizopo na kuungana pamoja ili kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hapo 24,11,

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!