Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

ONGEZEKO LA MISIKITI KAHAMA LACHANGIA KUPUNGUZA MAUAJI YA VIKONGWE NA WATU WENYE UALBINO.

SHEHE MKUU WA WILAYA YA KAHAMA OMARY DAMKA
KAHAMA 
Kuongezeka kwa maeneo ya kuabudia hususani Misikiti wilayani Kahama mkoani Shinyanga kumetajwa kupunguza jamii kutenda vitendo vya ukatili kama vile mauaji ya vikongwe na watu wenye ualbino kutokana na watu kuwa na hofu ya Mungu.

Hayo yamebainishwa leo na Sheikh wa wilaya ya Kahama Alhaj Omari Damka kwenye hafla maalumu ya Ufunguzi wa Msikiti wa Ijumaa uliopo katika Mtaa wa Mbulu katika Halmashauri ya Mji wa Kahama.

Amesema kwa sasa mauaji hayo yamepungua kutokana na jamii kuachana na vitendo vya ukatili vilivyokuwa vikichangiwa na imani potofu kuhusiana na wazee na watu wenye ulemavu wa ngozi katika mkoa wa shinyanga.

Sheikh Damka amesema viongozi wa dini wanajukumu kubwa la kuibadilisha jamii kwa kuhakikisha inakuwa na amani na kuendelea na shughuli za uzalishaji mali ambazo zitawasidia kupata vipato halali katika familia zao.

“Jamii inapaswa kuacha dhana hiyo potofu na badala yake wadumishe amani ikiwa ni pamoja na kuunga mkono shughuli zinazotekelezwa na serikali ya awamu ya Tano chini ya Dk John Pombe Magufuli kwa kwenda kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura ambalo linaendelea wilayani humo”,alisema Sheikh Damka.

Naye Mwakilishi wa Jumuiya ya Kiislamu ya International Istiqaama Community, Sheikhe Ahmed Mohamed Alhapsy amewataka waumini wilayani humo kuacha kubaguana na badala yake washirikiane katika kuijenga jamii ili iendelee kuwa na amani.

“Endapo Waislam wakianza kubaguana na kutoshirikiana kwa kigezo cha Madhehebu inaweza kukwamisha maendeleo ya dini sambamba kutofikisha ujumbe sahihi ambao wanapaswa kuutoa kwa waumuni wao”,alisema Ahmed.

Msikiti huo umejengwa kwa ufadhili wa Jumuiya ya Kiislamu ya International Istiqaama Community,chini ya Sheikh, Ahmed Haroun Alnooby.

MATUKIO KATIKA PICHA:


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News