Header Ads

NEC YAWATAKA WANAUME KAHAMA KUACHA TABIA YA KUWAZUIA WAKE ZAO KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUPIGA KURA.KAHAMA
Wito umetolewa kwa wanaume  nchini kuacha tabia ya kuwazuia wanawake kwenda kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kuwa  ni haki ya kila  mwananchi mwenye sifa ya kupiga kura kuwa na kitambulisho cha mpiga kura.

Wito huo umetolewa  leo mjini Kahama na afisa elimu tume  ya taifa ya Uchaguzi (NEC),  ROSE MALO wakati akizungumza kwenye kipindi cha Ukurasa mpya kinachorushwa na Kahama fm.

Amesema wapo baadhi ya wanaume wamekuwa wakiendeleza mfumo dume kwa kuwakataza wenza wao kujiandikisha kupata kitambulisho cha mpiga kura jambo ambalo ni kosa  kisheria na linamyima mwanamke haki ya msingi katika kuchagua viongozi ananaowataka.

Katika hatua nyingine Afisa kutoka NEC, MONICA WABUKUNDI amewataka wananchi wenye sifa ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi  katika maeneo ya kujiandikishia huku akiwataka Waandikishaji kutoa kipaumbele kwa makundi yanye uhitaji yakiwamo, ya wazee, watu wenye ulemavu, wajawazito na wenye watoto wadogo.

Zoezi la Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura  mkoani Shinyanga linatarajia kuanza  Septemba 20 hadi  hadi 26 mwaka baada ya kuharihsiwa  mara kadhaa.


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!