Header Ads

MWILI WA ALIYEWAHI KUWA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA SERIKALI YA AWAMU YA KWANZA, BALOZI IBRAHIM KADUMA KUZIKWA JUMATANO

Mwili wa aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Awamu ya kwanza, Balozi Ibrahim Kaduma, unatarajiwa kuzikwa Jumatano ya Septemba 05, 2019 Kijijini kwao Kibena mkoani Njombe.

Marehemu Kaduma amefariki Agosti 31,2019 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.
 Mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es Salaam.

Yohane  Kaduma, mtoto wa kiongozi huyo mstaafu akizungumza  leo Jumatatu Septemba 2, 2019 amesema kuwa kesho kuanzia saa mbili asubuhi itafanyika ibada fupi nyumbani kwao Makongo Juu.

Amesema baada ya ibada hiyo mwili utapelekwa katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) jijini Dar es Salaam,

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!