Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

MWANAFUNZI AJIUA BAADA YA KUZOMEWA NA WENZIE MWALIMU AKIMTAKA ATOKE DARASANI DAMU ZA HEDHI

Mwanafunzi mmoja nchini Kenya amejiua baada ya kudaiwa kuzomewa darasani kwa kuwa sare yake ya shule ilichafuka na madoa ya damu alipokuwa kwenye hedhi.

Mama wa Mwanafunzi huyo mwenye miaka 14 alisema binti yake alijinyonga baada ya kudhalilishwa na mwalimu wake, vyombo vya habari vya Kenya vimeripoti.

Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kutawanya kundi la wazazi takribani 200 waliokuwa wamepiga kambi nje ya shule, taarifa zinaeleza.

Kenya ilipitisha sheria mwaka 2017 kugawa taulo za kike bure kwa wanafunzi wa kike shuleni.

Mama wa binti huyo alisema mwalimu alimuita mwanafunzi huyo ''mchafu'' na kumtaka atoke nje shuleni Kabiangek, Magharibi mwa mji mkuu Nairobi, siku ya Ijumaa juma lililopita.

''Hakuwa na pedi. Na damu ilipochafua nguo zake, aliambiwa atoke darasani na asimame nje,'' mama yake alinukuliwa akiongea kwenye vyombo vya habari.

Alisema binti yake alirejea nyumbani na kumwambia mama yake kilichotokea shuleni, lakini alipokwenda kuchota maji alijinyonga.

Wazazi wake waliripoti tukio hilo polisi lakini imedaiwa hakukuwa na hatua zozote zilizochukuliwa, Gazeti la Daily Nation limeripoti.
Wasichana wa Turkana hukosa masomo wakati wa hedhi

Pamoja na wazazi wengine walikusanyika nje ya shule siku ya Jumanne. Polisi walifika na kuwakamata watu watano wakati waandamanaji walipofunga barabara na kuvunja geti la shule, ripoti zimeeleza.

Polisi wa mkoa Alex Shikond amesema mazingira ya kifo cha binti huyo yanachunguzwa.

Mkuu wa shule hiyo alikataa kuzungumza kuhusu tukio hilo.

Nchini Kenya na kwingineko, wasichana wengi hawawezi kumudu gharama za pedi.

Ripoti ya umoja wa mataifa ya waka 2014 ilisema kati ya wasichana kumi waishio kusini mwa jangwa la Sahara mmoja hukosa masomo wakati wa hedhi.

Baadhi ya wasichana hupoteza asilimia 20 ya masomo yao kwa sababu ya hedhi.
Chanzo - BBC

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News