Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

MTALII AFIA CHINI YA BAHARI ZANZIBAR AKIMCHUMBIA MPENZI WAKE

Mtalii mmoja aliyejulikana kwa jina la Steven Weber Jr, alifariki Dunia hivi karibuni akiwa chini ya Bahari alikoenda kumvisha pete mchumba wake, Kenesha Antoine wakati wa likizo.

Kulingana na mtandao wa Sky News, Steven Weber na Kenesha Antoine walikuwa wakiishi katika hoteli moja ya mbao ambayo ipo chini ya maji ya Bahari huko Visiwani  Zanzibar,  ili kuwawezesha kuona kilichopo maji.

Picha zimeonyesha wakati bwana Weber kutoka eneo la Baton Rounge mjini Luoisiana Marekani, alivyoogelea hadi katika dirisha moja lililopo chini ya maji kabla ya kushika karatasi akimuomba  Antoine akubali kufunga naye ndoa.

Karatasi hiyo ilisoma kwa tafsiri isiyo rasmi: “Siwezi kuzuia pumzi zangu kwa muda mrefu ili kukwambia kila kitu ninachokupendea lakini kila kitu ninachokupendea nakupendea kila siku”.

Bwana Weber baadaye aliibadilisha karatasi hiyo ili kuonyesha maneno aliyokuwa ameandika upande mwengine yaliosema: “Je tafadhali unaweza kuwa mke wangu? Utafunga ndoa nami???.

Kulingana na mtandao wa Sky News, baadaye alitoa pete ya uchumba kutoka katika mfuko wake kabla ya kuogelea na kuondoka eneo hilo.

Bi Antoine naye alichapisha picha za kisa hicho katika facebook ambapo anaonekana akifurahia pamoja na tamko lake: Ndio! Ndio! Ndio!.

Lakini mrembo huyo baadaye alichapisha habari mbaya kwamba mpenzi wake amefariki.

Bi Antoine alisema kwamba hakurudi akiwa mzima baada ya kuogelea baharini.

Wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani ilisema kwamba mtalii mmoja wa Marekani amefariki nchini Tanzania lakini hakuna maelezo zaidi yalioripotiwa.
tangazo

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News