Header Ads

MSANII MADEE AKATAZA NYIMBO ZAKE KUTOCHEZWA KWENYE VYOMBO VYA HABARI

Msanii wa Bongo Fleva, Madee ametangaza nyimbo zake zote alizozifanyia nchini Afrika Kusini kutochezwa tena kwenye Vyombo vya Habari.

Amefikia uamuzi huo kufuatia kuibuka kwa vurugu katika nchi hiyo ambapo raia wa kigeni ambao wamekuwa wakifanya biashara katika miji mikubwa kuporwa mali zao.

"Kwa hiari yangu nimeamua kuzuia kuchezwa kwa nyimbo zangu ambazo nimezifanya kwenye ardhi ya Afrika Kusini hasaVUVULA na zingine zisipigwe kwenye kituo chochote cha habari na zaidi ikiwa ni ni TV, Kwa sababu TV ndio kitu kinachoonyesha mandhari ya nchi tajwa ambayo ni SA, Binafsi nimechukua hatua kwanza kwa kuufuta hata kwenye channel yangu ya Youtube ambako ulikua unapatikana," ameeleza.

Amesema wakati anatoka Tanzania kwenda Afrika Kusini kufanya video ya wimbo huo lengo lake lilikuwa kutangaza vivutio vya Afrika kwa ujumla, Kwa kuwa anaamini Waafrika ni Wamoja.

"Nimefikia hatua hii kwa sababu kuu mbili, kwanza kile kinachoendelea kwasasa kila mtu anajua namna Waarika Kusini wanachowafanyia Waafrika wenzetu. Pili kumuenzi Mzee wetu MUGABE ambae wengi wetu humu tunajua historia yake ya kupambania mtu mweusi (Mwafrika)na miongoni mwa watu waliokua wakipinga utawala wa watu weupe alikua anapambana kuhakikisha Waafrika tunajikomboa" amesema Madee.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!