Header Ads

MKANDA WA SAUTI KUHUSIANA NA MAUJI YA MWANDISHI WA HABARI JAMAL KASHOGGI WAACHIWA


Gazeti la Sabah la kila siku nchini Uturuki limeachia mkanda wa sauti uliorekodiwa kati ya Mwandishi wa Habari Jamal Kashoggi na kikundi cha mauaji kinachosadikiwa kumuua na kumkata kata ndani ya Ubalozi wa Saudia mjini Instanbul.

Sauti hizo zinazoaminika kurekodiwa na Shirika la Ujasusi la Uturuki, zimeachiwa hadharani hapo jana zikiangazia mazungumzo kati ya watu wanao sadikika kumuuua mwanahabari huyo tangu akiwasili ubalozini na mpaka mauaji yake kisha mwili kukatwa vipande na kutolewa ndani ya ubalozi huo ukiwa kwenye masanduku matano.

Katika mfululizo wa majadiliano ya sauti hizo, mmoja ya wanaoaminika kuwa alitumwa kumuua Jamal Kashoggi, alisikika akisema kwamba yeye hupenda kusikiliza muziki anapokua anafanya mauaji kisha hunywa kahawa na kuvuta sigara.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!