Header Ads

MAMLAKA YA HALI YA HEWA KUTANGAZA UTABIRI WA MVUA ZA VULI


Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini(TMA), leo itatoa utabiri wake wa msimu wa Mvua za Vuli kwa kipindi cha Oktoba, Novemba hadi Disemba mwaka huu.

Mkurugenizi wa TMA, Dkt.Agnes’s Kijazi amesema hayo wakati akifungua warsha ya siku moja kwa aandishi wa Habari iliyofanyika leo katika Makao Makuu ya TMA, Ubungo jijini Dar ea Salaam.

Amesema, kwa kuzingatia umuhimu wa taarufa za hali ya hewa, mamlaka haina budi kutoa taarifa zake mapema na kwa wakati ili ziweze kufikia wananchi wote na sekta husika kwa ajili ya kuwawezesha kuchukua hatua stahiki ikiwemo kuepukana na majanga yanayoweza kusababishwa na mvua kwa kuwa matumizi ya taarifa za hali ya hewa kwa jamii katika shughuli zetu za kila sik ni ya muhimu.

Amesema, TMA, imekuwa ikahakikisha inakutana na wanahabari ambao ni daraja muhimu kati ya taasisi zetu za serikali na wananchi wote kwa ujumla katika kuwapa warsha mbali mbali za kujadili mwelekeo wa msimu wa Mvua na kuongeza kuwa Serikali ya Awamu ya tano inatambua vyema mchango wa huduma za hali ya hewa nchini na umuhimu wa kuwafikia wananchi kwa wakati.

Dkt, Kijazi Amesema, lengo la warsha ya lei ni kujadili Mwelekeo wa Msimu wa Mvua za vuli kwa kipindi cha Oktoba hadi Disemba mwaka huu na kujadili athari zinazoweza kujitokeza, hivyo wataalamu wameandaa rasimu ya mwelekeo huo na viashiria vilivyopelekea kupatikana kwa utabiri huu,

Aidha amesema kutokana na maoni ya wanahabari na wadau wengine kuhusu lugha inayotumika kuwasilisha taarifa za hali ya hewa.

Mamlaka kwa kushirikiana na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na taasisi zingine ikiwemo BAKIZA na vyuo vikuu, imeweza kutafsiri baadhi ya maneno kwa lugha ya Kiswahili hivyo kupitia warsha hiyo wanahabari wamepata fursa ya kuona baadhi ya misamiati ya hali ya hewa iliyo katika lugha ya Kiswahili kwa lengo la kutoa maoni kabla haijaanza kutumika rasmi.

“Lugha ya kiswahili itasaidia wananchi kwa wingi, kuelewa utabiri wa hali ya hewa pale unaposomwa kwabi wakati mwingine imesheheni maneno ya kisayansi na yasiyo rahisi kueleweka na jamii,,” amesema Dkt.kijaz

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!