Header Ads

MAKONDA AWATAKA WATUMISHI WA MUNGU WAKAHUBIRI KATIKA KUMBI ZA STAREHE (CLUB)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amewaambia watumishi wa Mungu wenye nia ya kwenda kutoa mahubiri yao katika kumbi za starehe (klabu),  wamjulishe kuanzia wiki ijayo ili awape vibali.


Makonda ameyabainisha hayo leo Septemba 8, katika ibada ya Jumapili inayotolewa na Mtume Boniface Mwamposa, ambapo amesema kuwa ipo haja ya neno hilo kuenezwa maeneo yote na kuwafikia hata wa kwenye kumbi hizo kwa madai ya kwamba wanaoenda klub hawamjui Mungu.

''Mtumishi wa Mungu yeyote akitaka klabu ruksa, sasa nimuone huyo mtu mwenye klabu akatae mimi si ndio mkuu wa Mkoa, kuanzia wiki ijayo mkitaka kwenda klabu yoyote mniambie mkapige japo kwa nusu saa'' amesema Makonda.

Makonda ameongeza kuwa ni heri wawafuate huko huko maeneo yao ya starehe, wakalipate neno la Mungu ili siku ya mwisho wakuiulizwa wasije kusema hawakusikia.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!