Header Ads

MAJERUHI WENGINE WA AJALI YA MOTO MOROGORO WAFARIKI DUNIA

Majeruhi wengine wawili kati ya 13 waliokuwa wanatibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, kutokana na ajali ya moto ya Mjini Morogoro, wamefariki Dunia na mpaka sasa jumla ya vifo imefikia 104.

Akizungumza leo Jumapili Septemba 1, 2019, mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa MNH, Aminiel Aligaesha amesema Asha Ally Seleman (28) alifariki Jumatano iliyopita ya Agosti 28, 2019 na Avelina Pastory Aman (30) alifariki jana Jumamosi Agosti 31,2019.

Amesema majeruhi 11 ndio wamebaki hospitalini hapo kati ya 47 waliopokelewa tangu ajali hiyo ilipotokea ambapo 36 wamefariki.

Aligaesha amesema kati ya majeruhi 11 wanaoendelea kutibia MNH sita wapo wodi 22 ya Sewahaji na watano wako Chumba cha ungalizi maalum (ICU).

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!