Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

LEMBELI AWASHUKIA WAANDISHI WA HABARI WANAOKIUKA MAADILI.


MKURUGENZI WA KAHAMA FM,DAUDI JAMES LEMBELI.

DAR ES SALAAM
Waandishi wa habari nchini wametakiwa kutumia kalamu zao vizuri ili kuisaidia jamii yenye maisha duni waweze kufikiwa na huduma bora za kibinadamu na kuacha tabia ya kuwa vibaraka na wandishi wa watu matajiri wanaowaamuru waandike mambo wanayotaka wao.

Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa Kahama Fm,ambaye alikuwa mbunge wa zamani wa jimbo la Kahama Daud James Lembeli alipoalikwa na Shirika la Utangazaji la BBC London katika mahojiano Maalum.


Lembeli amesema waandishi wengi hivi sasa wamekuwa ni waandishi wa watu binafsi na siyo jamii hali inayowafanya waandike habari za kumsifia mtu huyo kwa maslahi yake binafsi huku jamii yenye matatizo ikiichwa bila mtetezi.

Ameongeza kuwa Mwandishi bora wa habari ni yule anayefuata maadili ya kazi yake na kuzingatia weledi wa taaluma hiyo ikiwa ni pamoja na kuleta mabadiliko  katika jamii kwa kuandika habari zinazoweza kuchochea maendeleo.
Sambamba na hayo Lembeli ameongeza kuwa jamii ina imani na waandishi wa habari ila imani hiyo inazidi kupungua kutokana na vitendo vya baadhi ya waandishi kuandika kwa ajili ya matumbo yao kwa manufaa ya wachache na siyo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Kuhusu Swala la Utunzaji wa mazingira,Lembeli amesisitiza watu kutokata miti na kuchoma misitu ovyo kwani misitu ni makazi ya wanyama ambao wengi wao ni vivutio vya watalii katika nchi yeu wakiwemo Sokwe ambao wanapendwa sana na wazungu.


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News