Header Ads

KACU:HAKUTAKUWA NA KIKAO CHA KUJADILI TUMBAKU YA ZIADA ILIYOZALISHWA NJE YA MKATABA.


MWENYEKITI WA KACU EMMANUEL CHEREHANI
KAHAMA
Chama kikuu cha ushirika wilayani Kahama mkoani Shinyanga (KACU) kimesema hakutakuwepo na kikao  chochote cha kujadili  tumbaku ya ziada  inayozalishwa  nje ya mkataba katika msimu 2019/2020.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Kahama na Mwenyekiti wa KACU EMMANUEL CHARAHANI wakati akizungumza kwenye kipindi cha   Ukurasa mpya kinachorushwa na Kahama fm siku ya Jumatatu hadi Ijumaa.

CHARAHANI amewataka Wakulima wa Tumbaku kulima  kwa kuzingata taratibu zilizowekwa ambapo kwa wilaya ya Kahama  jumla ya  kilo milioni 6.3 za tumbaku zinatarajiwa kuzalishwa ndani ya mkataba.
Katika hatua nyingine Charahani amesema zaidi ya kilo milioni mbili za tumbaku zimebaki kwa wakulima kutokana na kuzalishwa nje ya mkataba  katika msimu wa 2018/2019, ambapo kuanzia kesho wanatarajia kuanza ziara katika maeneo ya wakulima ili kutoa elimu ya kuzingatia kilimo cha mkataba.

Zao la Tumbaku ni miongoni mwa mazao  ya kibiarasha ambapo kwa wilaya ya Kahama idadi kubwa ya wakulima inatoka katika  halmashauri ya Ushetu.


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!