Header Ads

INDONESIA: POLISI WAMUHOJIANO WIZI WA SIMU KWA KUTUMIA NYOKA

Polisi nchini Indonesia imeingia matatani baada ya kusambaa kwa video moja mtandaoni ikiwaonyesha askari polisi wakimfanyia mahojiano mshukiwa wa wizi wa simu kwa kutumia nyoka.

Video hiyo inamuonesha mshukiwa huyo akiwa amefungwa pingu, huku askari akimsogezea nyoka huyo usoni na akisika akisema kwamba endapo hata kiri basi angemuwekea nyoka huyo sehemu za siri.

Taarifa ya msemaji wa polisi nchini humo imesema kwamba nyoka huyo hakuwa na sumu na endapo watajiridhisha basi askari waliohusika watachukuliwa hatua

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!