Header Ads

IFIKAPO DEC 31 KAMA HUNA CHOO MKOANI SHINYANGA FAINI LAKI TANO.

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA BI ZAINAB TELACK 
KAHAMA:
SERIKALI mkoani Shinyanga imesema kuwa ifikapo December 31 itaanza kuwachukulia hatua wananchi ambao hawatakuwa wamejenga vyoo bora ikiwa ni pamoja na kuwatoza faini ya shilingi Laki tano.

Hayo yamesemwa leo mjini Kahama  na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi Zainab Tellack  katika kilele cha kufunga kampeni ya Nyumba ni Choo iliyofanyika katika kata ya Majengo.

Tellack amesema kuwa baadhi ya wananchi hawana vyoo bora huku  wana uwezo wa kuvijenga na kwamba kufikia December 31 wataanza kuchukuliwa hatua jambo ambalo wananchi wilayani Kahama wameliunga mkono.

Sambamba na hayo Tellack amewataka wananchi kuacha tabia ya kujisaidia vichakani na kwamba wanawe mikono kwa maji safi na sabuni pindi wanapotoka kujisaidia.

Kwa upande wake Mratibu mkuu wa kitaifa wa Kampeni ya Usichukulie poa nyumba ni Choo Anyitike Mwakitalima amesema kuwa kati ya watu 100 wanaotoka chooni ni watu 20 tu wanaonawa mikono huku kila baada ya dakika 1 watu wanne wanafariki duniani kwa kula kinyesi cha binadamu.

Kampeni ya Usichukulie poa nyumba ni choo iliyoongozwa na balozi wa kampeni hiyo Mrisho Mpoto imehitimishwa leo wilayani Kahama mkoani Shinyanga huku mikoa 11 ikifikwa na kampeni hiyo.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!