Header Ads

HALMASHAURI YA KAHAMA MJI,IMEJIPANGA KUHAKIKISHA MTIHANI WA DARASA LA SABA UNAFANYIKA BILA UDANGANYIFU.


Na Ndalike Sonda (Kijukuu Blog)
Kahama
Halmashauri  ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga imesema imejipana  kikamilifu  ili kuhakikisha Mtihani wa taifa wa kuhitimu elimu ya Msingi kwa wanafunzi wa darasa la Saba unafanyika kwa ubora  bila udanganyifu wowote.

Hayo yameelezwa na Afisa elimu wa Shule za Msingi wa halmasahuri hiyo ALUKO LUKOLELA wakati akizungumza na Kijukuu Blog ambapo amesema  watahiniwa  wote 5,486 kutoka shule 72 za msingi wameandaliwa vya kutosha kwaajili ya kukabiliana na Mtihani huo wa Taifa.

Amesema mwaka huu halmashauri hiyo imejiwekea malengo ya kufaulisha  kwa asimilia 85, kutoka asilimia 65 waliyoipata   mwaka uliopita,  ambapo katika kufananikisha hilo  amewataka wadau wa elimu, wazazi na walezi kujipanga kutimiza mahitaji muhimu ikiwamo  chakula na usafiri kwa watahiniwa.

LUKOLELA amewataka pia walimu wasimamizi kufuata taratibu za baraza la mitihani Tanzania (NECTA) katika kusimamia Mtihani huo na kwamba  watahiniwa  nao waondoe hofu juu ya mitihani  huo wa kuhitimu elimu ya Msingi mwaka huu.

Mtihani wa Taifa wa darasa la Saba  nchini unatarajiwa kufanyika  kwa siku mbili kuanzaia Septemba 11 na 12 mwaka huu.


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!